Na, Costantine James Geita.
Wahamiaji haramu 77 Raia wa Burundi wamekamatwa mkoani Geita kwa kosa la kuingia nchini kinyume na sheria huku wakijihusisha na shughuli za kuendesha Baisikeli mkoani humo.
Wahamiaji hao wamekamatwa katika maeneo mbali mbali mkoani Geita kufuatia oparesheni inayoendeshwa mkoani Geita na idara ya uhamiaji kwa lengo la kuwabaini raia wa kigeni walioingia nchini kinyume na sheria.
Afisa uhamiaji Mkoa wa Geita kamishina msaidizi wa uhamiaji Emmanuel Lukumai amesema mpaka sasa wamekamata raia wa Burubdi 77 wanao endesha baisikeli huku wengine wakifanya shughuli mbalimbali za mashambani ambao wameingia nchini kinyume na sheria.
Kamishina Emmanuel amesema Raia hao wameingia nchini kinyume na sheria za nchi kwa lengo la kujishughulisha na shughuli mbali mbali ikiwemo kuendesha baiskeli nakufanya shughuli za mashambani.
Amesema wahamiaji hao baadhi yao watafikishwa mahakamani huku wengine watatozwa faini maarumu kamishina Emmanuel amewataka wakazi wa mkoa wa Geita kuacha tabia ya kuishi na Raia wa kigeni kinyume na sheria.
“Wito wangu kwamba wasipende kukaa na raia wa kigeni ambao hawajafata taratibu kama anamhitaji mtu afate taratibu zote za kiuhamiaji anapokuwa nchini” Amesema Afisa uhamiaji Mkoa wa Geita kamishina msaidizi wa uhamiaji Emmanuel Lukumai.
Wizey Yohani, Ninyonzima Khalfani na Nyawenda Rajabu, Ni miongoni mwa Raia 77 wa Burundi waliokamatwa mkoani Geita wamekili kuingia nchini Tanzania kinyume na taratibu za uhamiaji wamesema sababu za kuzamia nchini Tanzania ni maisha magumu waliyo nayo.