Home LOCAL MIAKA 60 YA MAPINDUZI NA MUUNGANO WA TANZANIA MAENDELEO NI MENGI-DK.MWINYI

MIAKA 60 YA MAPINDUZI NA MUUNGANO WA TANZANIA MAENDELEO NI MENGI-DK.MWINYI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania maendeleo mengi yamepatikana katika sekta tofauti zikiwemo za kijamii, kiuchumi , kisiasa na kidiplomasia.

 


Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipofungua Kongamano la kumbukumbu ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania lililoandaliwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar (IPA) kwa kushirikiana na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.Salim Ahmed Salim(CFR) kutoka Dar es Salaam katika ukumbi wa Dkt.Mohamed Ali Shein Kampasi ya Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe: 11 Juni 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ametoa rai kwa washiriki wa kongamano hilo kuzungumzia sera zinazopewa kipaumbele katika mipango mikuu ya Serikali zikiwemo za Uchumi wa Buluu, Uwekezaji, Diplomasia ya Uchumi na kutoa mapendekezo yao kwa Serikali.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kujenga jengo la Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar (IPA).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here