Home BUSINESS TCCIA MANYARA YATOLEA UFAFANUZI JUU YA ALIYEHUKUMIWA KUGHUSHI NYARAKA KUWA SIO MUAJIRIWA...

TCCIA MANYARA YATOLEA UFAFANUZI JUU YA ALIYEHUKUMIWA KUGHUSHI NYARAKA KUWA SIO MUAJIRIWA WAO KWASASA.

Na: Mwandishi Wetu ,Manyara.

Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilmo Mkoa wa Manyara (TCCIA Manyara) kimekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni zikimtaja mshauri wa biashara na mwajiriwa wa TCCIA Manyara Bw. Ramadhani Rashid Msangi kuhukumiwa kwenda jela miaka 3 au kulipa faini ya shilingi 900,000 kwa kosa la kughushi nyaraka za mafunzo kwa wajasiriamali mwaka 2018 hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Manyara tarehe 23 March 2024. Ambapo Chama hicho kimedai kuwa licha ya tuhuma zinazomkabili Bw.Ramadhani Rashid Msangi, kwa sasa sio mwajiriwa wa Chama hicho kwani aliondolewa kazini tangu April 2019 .

Taarifa kwa vyombo vya habari imetolewa na Uongozi wa Chama hicho ikieleza kuwa Mfanyakazi huyo aliondolewa miaka kadhaa iliyopita na tangu wakati huo hahusiki na shughuli zozote za Chama hicho. Chama Chetu TCCIA, kinaendelea kufanya kazi kwa uwazi na kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa katika katiba yetu. Tunajitahidi kufuata miongozo na mifumo iliyoainishwa katika katiba yetu, pamoja na kuzingatia sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunathamini uwazi na uwajibikaji katika kazi zetu, na tunajitahidi kuhakikisha kwamba tunazingatia viwango vya juu vya maadili na utawala bora katika kila hatua tunayochukua.(Mwenyekiti TCCIA Manyara)

Previous articleWAZIRI  MAMBO YA NJE WA HUNGARY  AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Next articleKAMATI YA PIC YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA JENGO LA PSSSF COMMERCIAL COMPLEX
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here