Home LOCAL MULILO ATANGAZA NJIA UTAKAPOPITA MWILI WA RAIS MSTAAFU HAYATI ALI HASSAN MWINYI...

MULILO ATANGAZA NJIA UTAKAPOPITA MWILI WA RAIS MSTAAFU HAYATI ALI HASSAN MWINYI KWENDA UWANJA WA UHURU

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muriro ametaja maeneo ambayo Mwili wa Hayati Rais Ali Hassan Mwinyi utapita ukiwa uneaelekea uwanja wa Uhuru kwaajili ya kuagwa na viongozi mbalimbali wa serikali, Taasisi, dini pamoja na wananchi.

Ametaja njia hizo ambazo zitatumika zitakuwa mbili njia ya kwanza ni kutoka Mikocheni watapita Shoppers Morocco lakini watakwenda msikitini kwaajili ya Ibada.

“Tukitoka kwenye ibada tutarudi kutoka Morocco kwenda Magomeni tutapita Manyanya, Mkwajuni hadi Kigogo tutapita karibu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam hapo tutakwenda hadi Veta hadi Chuo Kikuu Shirikishi cha Elimu Darr es salaam (DUCE) na kuishia Uwanja wa Uhuru,”amesema Muriro.

Amesema hizo ndio njia watakazatumia hivyo wananchi watakaopenda kuwa barabara kuaga mwili wa Hayati Mwinyi utapita njia hizo.

Ameongeza kuwa polisi na vyombo vingine vya dola wamejipanga kwenye maeneo hayo na utaratibu mzuri utakuwepo pale uwanjani ndani na nje.

Previous articleRAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MH DKT. MWINYI APOKEA WAGENI MBALIMBALI
Next articleWAZIRI MKUU AKIMPA POLE RAIS WA ZANZIBAR Dkt. HUSSEIN MWINYI MIKOCHENI DSM

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here