Home ENTERTAINMENTS WAREMBO WA BINTI AFRIKA WAANZA KUTIFUANA VIKALI KUELEKEA UZINDUZI MWEZI UJAO

WAREMBO WA BINTI AFRIKA WAANZA KUTIFUANA VIKALI KUELEKEA UZINDUZI MWEZI UJAO

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni KL International Argency, Alfonce Mkama Ntare Akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano huo.
Warembo zaidi ya ishirini wako kwenye mazoezi makali ndani ya Hoteli ya Kingazi Resort iliyopo Kijichi Mgeni Nani jijini Dar,es salaam ili kujiandaa na shindano la uzinduzi linalotarajiwa kufanyika Ukumbini hapo Machi 9 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete.
Akizungumza na wanahabari, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni KL International Argency, Alfonce Mkama Ntare waandaaji wa kinyang’anyiro hicho amesema maandalizi yote yameshakamilika na kinachosubiriwa ni siku tu na saa.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika mapizi tofauti tofauti
Mkurugenzi huyo lengo kubwa la shindano hilo ni kukuza lugha ya kiswahili pamoja na maadili ya kiafrika ambapo vigezo vyote hivyo vitazingatiwa katika kumpata mshindi. 
Ameendelea kusema kuwa shindano ambalo wengi hulifananisha na mashindano mengine ya mamiss lina utofauti mkubwa ambapo hili haliwatumii warembo waliokonda au wembamba kwakuwa kukonda au wembaba siyo kiwakirishi cha binti wa kiafrika. Ameendelea kusema.
Mkurugenzi wa Kingazi Resort, Yeriko Asiphiwe Mahenge Akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.
“Hili ni shindano la mabinti wenye shepu zao za kiafrika haswa maana wengine wanalifananisha shindano hili na mashindano mengine ya mamiss ambayo huwakilishwa na warembo wembamba.
“Kwa kusema hayo naomba wananchi wajiandae kushuhudia shindano hilo linalotarajiwa kuleta mageuzi makubwa na kutoa ajira na kubadilisha maisha ya mabinti hao”.
Mkama alimalizia kwa kusema baada ya kinyang’anyiro cha uzinduzi fainali yenyewe itakayowakutanisha mabinti kutoka mataifa mbalimbali Barani Afrika inatarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kingazi Resort, Yeriko Asiphiwe Mahenge inayotumika kama kambi ya mabinti hao na linapotarajiwa kushindano la uzinduzi amesema hoteli hiyo ina utulivu mzuri unaowafanya mabinti hao kuwa kambini kiusalama na amani huku wakitunzwa kwa huduma bora za vyakula, vinywaji na malazi safi. Mkurugenzi huyo amewakaribisha wananchi wengine kufika hotelini hapo kujipatia huduma bora na ya kisasa inayokwenda na wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here