Home LOCAL KINGAZI HOTEL INAWATAKIA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA HERI YA MIAKA 60 YA...

KINGAZI HOTEL INAWATAKIA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA HERI YA MIAKA 60 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR 

Mkurugenzi wa Kingazi Hotel Nelson Mahenge Akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati akiwatakia Watanzania maadhimisho mema ya siku ya mapinduzi ya Zanzibar

Na.Mwandishi wetu

Katika kuadhimisha siku ya mapinduzi ya Zanzibar Mkurugenzi wa Hoteli ya Kingazi Nelson Mahenge amewatakia heri Watanzania na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwenye maadhimisha miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema anawapongeza maraisi hao kwa Kazi kubwa wanayoifanya katika kuiongoza Nchi na kuijenga hivyo amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi ili mafanikio makubwa zaidi yaweze kupatikana

“Katika hotel hii ndipo itakapowekwa kambi ya binti Afrika, ambapo itachukua miezi minne hivyo tumejiandaa kupokea ugeni mkubwa kutoka Nchi mbalimbali za Afrika na kuahidi kutoa huduma Bora zaidi na usalama wa kutosha kabisa.

Mfano wa mabinti wenye maumbo ya asili, rangi pamoja na nywele za asili watakaokwenda kushindana mashindano hayo ya Binti Afrika

“Sisi tunapatikana maeneo ya Kijichi, Mgeni nani na nawakaribisha wageni na tupo tayari kuupokea ugeni huo,hapa tuna kila kitu ikiwemo malazi,chakula na vinywaji hivyo ukifika huduma zote zinapatikana nawaombea kila la heri washiriki wote ambao watakwenda kushiriki katika mashindano hayo, amesema,”Mahenge

Previous articleRAIS DKT.MWINYI AKUTANA NA MWENEZI MAKONDA IKULU ZANZIBAR
Next articleKILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here