Home BUSINESS TANAPA YANADI UPEKEE WA VIVUTIO VYA UTALII TANZANIA, YAJA NA TWENZETU...

TANAPA YANADI UPEKEE WA VIVUTIO VYA UTALII TANZANIA, YAJA NA TWENZETU MBUGANI

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) imenuia kuhamasisha utalii wa ndani ili kuleta maendeleo na mafanikio makubwa katika sekta hiyo inayoongozwa kwa kuleta fedha nyingi za kigeni.

“Msimu huu wa siku kuu za noeli (Christmas, Boxing Day) na mwaka mpya, tunawakaribisha watanzania kutoka sehemu kona zote za nchi kutembelea hifadhi zetu zilizosambaa nchi nzima”alisema Kaimu Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Juma Kuji

Alieleza “Kwa watu wa kusini wanaweza kwenda hifadhi za Mwalimu Nyerere au Mikumi au Ruaha, kwa watu wa Dar es salaam wanaweza kwenda Saadan au mkomazi au popote,”

Alisema “Kwa watu wa kigoma na congo wanaweza kwenda Gombe na mahale, kwa walio nyanda za juu kusini tunawakaribisha Kitulo na katavi sambamba na walioko magharibi ya katikati ambao tunawakaribisha waende Tabora hifadhi ya Mto ugala”.

Alifafanua “Kwa upande wa kanda ya ziwa wanaweza kwenda kuburudika Rubondo ama SAA nane au burigi chato, wanaweza pia kwenda ibanda kyerwa na rumanyika karagwe ambako kote huko watakutana na mandhari mazuri ya kuvutia”. Ameendelea kuwakaribisha Kuji

Alisema “Ukienda kaskazini utakutana na hifadhi maarufu za Serengeti, Ziwa manyara, Tarangire, hifadhi ya Taifa Arusha, mlima Kilimanjaro na Mkomazi hifadhi yenye faru wa aina yake”. Ameendelea kutaja utajiri wa hifadhi za Taifa

Kaimu Kamishna Kuji, alisema watanzania wanapaswa kutembelea vivutio vya utalii ambavyo vipo vya kipekee maeneo mbalimbali ya nchi kwa kila kanda.

Hivyo, alisema TANAPA imenuia kuhakikisha kufikia lengo la kuwa na watalii milioni 5, hivyo watanzanoa wajitokeze kwa wingi kutembelea vivutio vya utalii ambavyo vipo maeneo mbalimbali.

Previous articleMAKAMBA: MCHAKATO WA DIASPORA KUPEWA HADHI MAALUM KUKAMILIKA 2024
Next articleRAIS DKT. SAMIA KWENYE TUZO ZA WAZALISHAJI BORA WA BIDHAA TANZANIA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here