Home LOCAL MAKAMBA: MCHAKATO WA DIASPORA KUPEWA HADHI MAALUM KUKAMILIKA 2024

MAKAMBA: MCHAKATO WA DIASPORA KUPEWA HADHI MAALUM KUKAMILIKA 2024

 Na: Avila Batwely Greenwaves Media

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January, Makamba amesema mchakato wa hadhi maalum kwa watanzania waishio nje ya nchi (diapora) utakamilika mwaka 2024.

Akizungumza Leo Disemba 17 2023jijni Dar es Salaam na waandishi wa Habari Waziri Makamba wakati akieleza mafanikio ya ziara za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na tathimini ya diplomasia ya Tanzania kikazi.

Amesema katika kuhakikisha Hilo wamefanya mabadikiliko kifungu Cha Sheria ya uhamiaji kinachohusu suala la hadhi maalum katika bunge lijalo.

“Tutangaza hadhi maalumu na stahili mahususi kwa watanzania wanaoishi nje waenye asili ya Tanzania ambao Wana uraia wa nchi nyingine kuanza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo ya nchi yao,”amesema Makamba.

Amesema hadhi maalumu itaanza kutumika mwakani ambapo kupitia hadhi hiyo ya watanzania wataanza kushiriki kikamilifu katika mchakato wa maendeleo ya Tanzania, pia na ustawi wao binafsi ambao unawaunganisha wao na nchi yao.

Makamba ameleza mambo makubwa matano waliyofanya mwaka huu ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji na kukuza kiwango cha utalii nchini na kutafuta fedha kwaajili ya kugharamia nchini mikpona faida kwaajili ya maendeleo.

Amesema kuongeza ushawishi katika masuala mtambuka yanayo hitaji ushirikiano wa kimataifa, kuimarisha ujirani mwema ushirikiano wa kikundi pamoja usalama, amani na siasa na kuimarisha uhusiano kati ya nchi yetu duniani na taasisi mbalimbali.

Aidha amesema kupitia ziara za Rais Dk Samia mwaka uliopita uwekezaji umekua kwa asilimia kubwa ajira na kipato kimeongezeka hivyo ni mafanikio makubwa sana.

” Mwaka ujao ni kuendeleza haya tuliofanya ikiwemo kukamilisha na kupitia sera mpya ya mambo ya nje kufungua Balozi mpya, “amesema.

Previous articleWAZIRI MKUU AREJEA NCHINI KUTOKA MADAGASCAR
Next articleTANAPA YANADI UPEKEE WA VIVUTIO VYA UTALII TANZANIA, YAJA NA TWENZETU MBUGANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here