SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) imenuia kuhamasisha utalii wa ndani ili kuleta maendeleo na mafanikio makubwa katika sekta hiyo inayoongozwa kwa kuleta fedha nyingi za kigeni.
“Msimu huu wa siku kuu za noeli (Christmas, Boxing Day) na mwaka mpya, tunawakaribisha watanzania kutoka sehemu kona zote za nchi kutembelea hifadhi zetu zilizosambaa nchi nzima”– alisema Kaimu Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Juma Kuji
Alieleza “Kwa watu wa kusini wanaweza kwenda hifadhi za Mwalimu Nyerere au Mikumi au Ruaha, kwa watu wa Dar es salaam wanaweza kwenda Saadan au mkomazi au popote,”
Alisema “Kwa watu wa kigoma na congo wanaweza kwenda Gombe na mahale, kwa walio nyanda za juu kusini tunawakaribisha Kitulo na katavi sambamba na walioko magharibi ya katikati ambao tunawakaribisha waende Tabora hifadhi ya Mto ugala”.
Alifafanua “Kwa upande wa kanda ya ziwa wanaweza kwenda kuburudika Rubondo ama SAA nane au burigi chato, wanaweza pia kwenda ibanda kyerwa na rumanyika karagwe ambako kote huko watakutana na mandhari mazuri ya kuvutia”. Ameendelea kuwakaribisha Kuji
Alisema “Ukienda kaskazini utakutana na hifadhi maarufu za Serengeti, Ziwa manyara, Tarangire, hifadhi ya Taifa Arusha, mlima Kilimanjaro na Mkomazi hifadhi yenye faru wa aina yake”. Ameendelea kutaja utajiri wa hifadhi za Taifa
Kaimu Kamishna Kuji, alisema watanzania wanapaswa kutembelea vivutio vya utalii ambavyo vipo vya kipekee maeneo mbalimbali ya nchi kwa kila kanda.
Hivyo, alisema TANAPA imenuia kuhakikisha kufikia lengo la kuwa na watalii milioni 5, hivyo watanzanoa wajitokeze kwa wingi kutembelea vivutio vya utalii ambavyo vipo maeneo mbalimbali.