Home LOCAL MSHINDI SHINDANO LA BINGWA KUONDOKA NA ZAWADI YA CRAWN

MSHINDI SHINDANO LA BINGWA KUONDOKA NA ZAWADI YA CRAWN

SHINDANO la Bingwa Msimu wa pili linalokutanisha Watu maarufu wa kwenye mitandao ya kijamii, Washiriki wabaki 12 waliofika final mshindi wa bingwa kuondoka na zawadi ya gari, aina ya crawn 

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Jijini Dar es salaam, Meneja Mradi wa shindano hilo Ombeni Phiri amesema bingwa ni zaidi ya burudani ambapo msimu wa pili mshindi kuondoka na gari aina ya crown pamoja na pesa taslim.

Msimu wa kwanza waliingia washiriki 18 ambao wengi wao ni vijana wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na mmoja wao aliibuka mshindi na gari aina ya crown pamoja na pesa taslim.

Hata hivyo ameeleza lengo la kuwepo kwa shindano hilo ni kuwapa fursa vijana Kujifunza vitu mbalimbali ikiwemo fursa zilizopo katika mitandao ya kijamii katika kukuza na kutengeneza majina (brand) yao.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza kuwa shindano hilo linasaidia kuwapa vijara ajira na kupata mitaji kupitia vipaji vyao.

Mshindi anakuwa balozi na anapewa taratibu jinsi ya kufanya biashara na kuweza kukuza na kujitamgaza.

Pia amesema Shindano hilo ni daraja la kufunguka kwa fursa nyingi kwani Hata usipofanikiwa kushinda unaweza kupata fursa ya kuwa balozi wa Makampuni.

Aidha Malisa amewaambia watazamaji wa bingwa kulipia visimbuzi vyao kwani msimu wa pili una maudhui tofauti tofauti yenye kufunza ambapo hata watazamaji watapata elimu mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here