Home BUSINESS ORYX YAGAWA BURE MITUNGI YA GESI KWA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO HANANG

ORYX YAGAWA BURE MITUNGI YA GESI KWA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO HANANG

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama ( kushoto) akiwa ameshikana mkono na Mkuu wa Idara ya Mauzo wa Oryx Gas Tanzania Shaban Fundi (kulia) baada ya Oryx kukabidhi mitungi 200 ya kilo 15 yakiwa na majiko yake kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh.

Na Mwandishi Wetu

MISAADA mbalimbali imezidi kutolewa kwa waathirika wa janga la maporomoko ya tope na mafuriko yaliyotokea wilayani Hanang, Mkoa wa Manyara na kusababiaha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu wa mali.

Katika kuunga mkono kuwafariji wananchi hao, Kampuni ya Oryx Gas Tanzania imetoa pole kwa wananchi walioathirika kwa kutoa mitungi ya gesi 200 yenye ujazo wa kilo 15 kuwsaidia katika kipindi hiki kigumu.

Mitungi hiyo ya gesi ikiwa na majiko yake, imetolewa imekabidhiwa kwa serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama na kushuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga.

Akizungumza wakati wa kupokea mitungi hiyo Waziri Mhagama ameishukuru kampuni ya Oryx kwa mchango wake kwa wananchi wa Hanang kwani umekuja wakati muafaka kusaidia wananchi hao kwa kuwapatia nishati safi ya kupikia katika wakati huu mgumu.

Mkuu wa Idara ya Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas, Shaban Fundi amesema kampuni hiyo imefika Hanang katesh kuungana na kuwapa pole watanzania wenzao waliofikwa na janga la mafuriko na maporomoko.

“Tunajua kwa hakika wenzetu wameathirika sana katika kipindi hiki ni gharama kubwa kupata vyanzo vya moto kupikia. Oryx Gas tumekuja kukabidhi majiko 200 na mitungi ya gas ujazo wa kilo 15 kwa waathirika wa tukio hili.

“Oryx Gas tunawaombea marehemu wapumzike kwa amani, zaidi tunawaombea majeruhi wote wapone haraka na werejee katika majukumu yao ya kila siku.”

Fundi amesisitiza kuwa kampuni hiyo itaendelea kuwa karibu na jamii ya Watanzania katika nyakati zote zikiwemo za majanga kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kusaidia ufumbuzi wa changamoto ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mwisho

Previous articleMSHINDI SHINDANO LA BINGWA KUONDOKA NA ZAWADI YA CRAWN
Next articleRAIS SAMIA ABAINISHA CHANGAMOTO ZINAZOPASWA KUPEWA KIPAUMBELE DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here