Home BUSINESS CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI CHATEMBELEA BENKI KUU DAR ES SALAAM

CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI CHATEMBELEA BENKI KUU DAR ES SALAAM

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi , Balozi Meja Jenerali Wilbert Ibuge, akikabidhiwa zawadi na Naibu Gavana wa BoT, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila, wakati wa ziara ya wanafunzi wa chuo hicho Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Naibu Gavana wa BoT, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila, akikabidhiwa zawadi na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi , Balozi Meja Jenerali Wilbert Ibuge, wakati wa ziara ya wanafunzi wa chuo hicho Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Naibu Gavana wa BoT, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila, akizungumza wakati akiukaribisha ujumbe wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi ulipotembelea Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Meneja, Utafiti kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Dkt. Deogratias Macha, akiwasilisha mada kuhusu Wajibu wa Benki Kuu katika kukuza usalama wa taifa kwa  ujumbe wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi ulipotembelea Benki Kuu jijini Dar es SalaamMkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi , Balozi Meja Jenerali Wilbert Ibuge, akikabidhiwa zawadi na Naibu Gavana wa BoT, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila, wakati wa ziara ya wanafunzi wa chuo hicho Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi , Balozi Meja Jenerali Wilbert Ibuge, akizungumza wakati wa ziara ya wanafunzi wa chuo hicho Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Utafiti and Sera za Uchumi, Dkt. Suleiman Missango, akizungumza wakati wa ziara ya wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wakifuatilia wasilisho kuhusu Wajibu wa Benki Kuu katika kukuza usalama wa taifa lililotolewa na Meneja, Utafiti kutoka Kurugenzi ya Utafiti and Sera za Uchumi, Dkt. Deogratias Macha.

Benki Kuu ya Tanzania kama mhimili wa mfumo wa fedha nchini ina mchango mkubwa kuhakikisha maendeleo na uhimilivu wa kiuchumi, ambayo ni misingi muhimu ya usalama wa taifa.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila amesema hayo wakati akiukaribisha ujumbe wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi ulipotembelea Benki Kuu jijini Dar es Salaam. Ujumbe huo uliongozwa na Mkuu wa Chuo hicho, Balozi Meja Jenerali Wilbert Ibuge, wakufunzi na wanafunzi 53.

Dkt. Kayandabila amesema, katika mazingira ya dunia ya sasa yanayobadilika, wajibu wa benki kuu duniani ni zaidi ya majukumu yanayohusu fedha.

“Sisi hapa Benki Kuu ya Tanzania tunaelewa sana kuhusu uhusiano wa karibu kati ya utulivu wa uchumi na usalama wa taifa letu kwa ujumla,” alisema na kuongeza kuwa uchumi imara siyo tu kwa ajili ya kukidhi malengo ya kifedha au kibajeti, bali pia ni muhimu sana katika usalama wa taifa.

Katika ziara hiyo, Benki Kuu ilifanya wasilisho kuhusu Wajibu wa Benki Kuu katika kukuza usalama wa taifa (Role of the Bank of Tanzania in promoting national security). Wasilisho hili lilifanywa na Meneja, Utafiti kutoka Kurugenzi ya Utafiti and Sera za Uchumi, Dkt. Deogratias Macha, na kufuatiwa na kipindi cha maswali na majibu kutoka kwa wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi.

Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilianzishwa mwaka 2012 na huwaleta pamoja maofisa wa ngazi za juu wa serikali na taasisi zingine kupata mafunzo ya kimkakati yanayohusu usalama wa taifa.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo ya mafunzo, Mkuu wa Chuo hicho Balozi Meja Jenerali Ibuge alisema kati ya wanafunzi 53, Watanzania ni 31 na maafisa waandamizi 22 wanatoka nchi marafiki barani Afrika na Asia.

Balozi Maj. Jenerali Ibuge alisema wanafunzi hao wameanza kujifunza masuala ya uchumi na uhusiano na usalama wa taifa na kuona ni muhimu kutembelea Benki Kuu ya Tanzania ili kujifunza kazi zake.

Ameishukuru Benki Kuu kwa kuwakaribisha na kueleza matumaini yake kwamba ushirikiano huo utaendelea.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Uthabiti wa Sekta ya Fedha, Bi Sauda Msemo, menejimenti na wafanyakazi kadha wa Benki Kuu pia walikuwepo kuwapokea wageni hao.

Chuo cha Taifa cha Ulinzi kinatoa mafunzo ya muda mrefu na ya muda mfupi yanayohusiana na usalama wa taifa.

Previous articleBRELA NA TAKUKURU YA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA UTENDAJI KAZI
Next articleMAJALIWA ASALIMIANA NA SUMAYE KATESH
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here