Home BUSINESS TADB YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO

TADB YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (usimamizi wa uchumi) Elijah Mwandumbya (kati kati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango Mkakati wa miaka mitano (2023-2027) pamoja na huduma mpya za kifedha za Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Frank Nyabundege na kulia ni Hawabai Abdulla ambaye ni afisa mwandamizi wa masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi kutoka TADB.

Na Mwandishi Wetu

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) limezindua Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2023-2027) pamoja na bidhaa mpya tatu za kifedha zinazolenga kuboresha kilimo hapa nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi wa Uchumi) Elijah Mwandumbya aliyemwakilisha Waziri wa fedha alisema Serikali inafahamu umuhimu wa Kilimo kwa uchumi wa nchi na kuutambua mchango wa TADB katika kutoa mikopo yenye riba nafuu kwenye kilimo na kuongeza kuwa Serikali itaendeleo kuwekeza kwenye kilimo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (usimamizi wa uchumi) Elijah Mwandumbya (wa pili kushoto), akionyesha mwongozo wa Mpango Mkakati wa miaka mitano (2023-2027) wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) muda mfupi baada ya uzinduzi wa mpango huo pamoja na bidhaa za kifedha za benki hiyo. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Frank Nyabundege (wa pili kulia). Wa Kwanza kushoto ni mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na wa Kwanza kushoto ni Daniel Masolwa, Mjumbe wa bodi ya TADB.

“Mwaka 2022/23, Serikali imewekeza jumla ya TZS 751.1 billioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 155.3% kutoka TZS 294.16 billioni ilizowekeza katika sekta ya kilimo mwaka uliopita. Ongezeko hili kubwa linadhihirisha wazi nia ya serikali kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya Kilimo” alisema.
Naibu Katibu Mkuu aliipongeza uongozi wa TADB pamoja na wafanyakazi kwa kukuza ufanisi wa benki hiyo kwa kuongeza wigo wa huduma zake, huku akiwahakikishia kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono.

Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Frank Nyabundege alifafanua kuwa Mpango Mkakati wa TADB wa Miaka Mitano 2023 – 2027 unalenga maeneo makuu matatu
“Eneo la kwanza ni kuleta chachu ya ongezeko la huduma za kifedha zinazotolewa na benki nyingine kwenda sekta ya kilimo, huku TADB ikiongoza katika utoaji wa huduma hizo. ,” alisema.
Eneo la pili alisema TADB itachangia ukuaji wa mnyororo wa ongezeko la thamani kwa kutumia fursa zilizopo ndani sekta ya kilimo ili kufanikisha uwekezaji zaidi katika miondombinu ya uzalishaji, mashine, uhifadhi wa mazao, uchakataji, huduma za kimkakati na biashara ya bidhaa,

Baadhi ya wageni waalikwa ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa taasisi za fedha na mabenki washirikia katika kutoa mikopo chini ya Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS) unaoendeshwa TADB wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu muda mfupi baada ya uzinduzi wa Mpango Mkakatii wa miaka mitano pamoja na huduma mpya za kifedha

Katika eneo la tatu alifafanua kuwa benki hiyo itazingatia kilimo cha kisasa kinachoendana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuandaa mikakati inayoshugulikia mabadiliko hayo na kuongeza uwezo wa wakulima kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Kwenye eneo la nne,tutaongeza ujumuifu kwenye hudumma za kifedha.TADB itaongeza idadi ya wanawake na vijana wanaojishugulisha na kilimo, ambapo kwa sasa wanawake ni asilimia 46% na vijana ni 44%.

Mwisho, katika eleo la tano, benki inajidhatiti kukuza uwezo wake kwa kujenga mahusiano chanya, kukuza rasilimali fedha kwa ajili ya kilimo, kupanua wigo wa huduma zake, kujenga uwezo wa uongozi, uadilifu, kupunguza athari na kuwekeza kwa watu na mifumo bora.,” alisema

Mkurugenzi huyo alisema kuwa TADB inaongozwa na mkakati wa muda mrefu wa miaka 20 wa kibiashara (2015-2035) ambao unatekelezwa kupitia mikakati ya kati ya miaka mitano mitano.

Previous articleWAUGUZI WATUHUMIWA KUOMBA RUSHWA KWA MAMA WAJAWAZITO.
Next articleSPIKA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKUTANA NA MAKONDA 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here