Home LOCAL WAUGUZI WATUHUMIWA KUOMBA RUSHWA KWA MAMA WAJAWAZITO.

WAUGUZI WATUHUMIWA KUOMBA RUSHWA KWA MAMA WAJAWAZITO.

 

Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa WA Tabora ,Musa Chaulo  Akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani .

Na: Lucas Raphael,Tabora

Baadhi ya Watumishi wa idara ya afya mkoani Tabora wanatuhumiwa kuomba Rushwa kutoka kwa kinamama wajawazito wanaohitaji huduma ya kujifungua na kutoa lugha mbaya kwa wateja wao wanapokuwa wanahudumiwa kwenye vituo vya afya na zahanati.

Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Tabora ,Musa Chaulo alitoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari mkoani hapa .

Alisema kwamba wauguzi hao wamekuwa wakiomba Rushwa kwa kinamama wajawazito jambo ambalo ni kinyume  na taratibu za wizara ya afya.

Alisema kwamba wauguzi hao wamekuwa wakipigana na urataribu wa serikali jambo ambalo wanaendelea kulifanyika kazi kupitia Takukuru Rafiki .

Chaulo  alisema licha ya kuomba Rushwa pia wamekuwa wakitoa Lugha mbaya kwa wagonjwa wanaokwenda kupata huduma za matibabu kwenye hospitali hizo .

Hata hivyo alisema wilaya mbili katika mkoa huo ndio kinara wa matukio hayo kwa zaidi ya kinamama 20 walitoa malalamiko juu ya kadhia hiyo ya kuombwa Rushwa na kutolewa kwa lugha mbaya .

Aidha alisema kwamba Takukuru Rafikia inaendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wanapinga vita matendo ya Rushwa pia kwa kushirikiana na jeshi la polisi .

Alisema kwamba jeshi la polisi zimeongezeka Doria na wale Askari polisi wanaomba Rushwa ili kutoa Dhamana kwa vitendo hivyo jeshi hilo limeanza uchukua hatua kwa Askari aliyejiuhusisha na utovu wa nidhamu lilimfikisha Takukuru ambapo alifunguliwa kesi ya jinai .

Hata hivyo kamanda huyo wa Takukuru mkoani hapa wanaendelea na elimu ya kuzuia rushwa kwa kuwafikia makundi mbalimbali ya kijamii .

Chaulo alisema kuwa wanadendela kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa kufuata sheria na kanuni na Taratibu .

Previous articleUTAFITI WA VIASHIRIA VYA VVU NA UKIMWI WAKAMILIKA HUKU UKIWA NA MATOKEO CHANYA.
Next articleTADB YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here