Home LOCAL REA: VIJIJI VYOTE KUFIKIWA NA UMEME IFIKAPO MWEZI JUNI,2024

REA: VIJIJI VYOTE KUFIKIWA NA UMEME IFIKAPO MWEZI JUNI,2024

Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huyo katika Kikao kazi na Wahariri wa Habari kilichofanyika leo Novemba 23-2023 Jijini Dar es Salaam, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Mbadala Jadidifu REA Mhandisi Aduera Mwijage akizungumza katika Mkutano wa Wahariri wa habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina leo Novemba 23, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Bw. Daudi Kosuri akizungumza katika Mkutano wa Wahariri mbalimbali wa habari ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina leo Novemba 23, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akizungumza kwa niaba ya Wahariri walioudhuria Kakao hicho.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kutekeleza Miradi saba yenye thamani ya zaidi ya Trillioni 1.5 kwaajili ya kufanikisha miradi ya nishati ya umeme vinijini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu alipokuwa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala huyo katika Kikao kazi na Wahariri wa Habari kilichofanyika leo Novemba 23-2023 Jijini Dar es Salaam, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Amesema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo inayoendelea inatokana na dhamira ya dhati ya Serikali katika kuhakikisha vijiji vyote vinapata umeme ifikapo mwaka 2025, lakini wanatarajia kuvifikia vijiji vyote 12,313 vya Tanzania Bara ifikapo mwezi Juni 2024.

“Tumepata Sapoti kubwa ya Serikali iliyotuwezesha kufanya kazi kwa bidii na kuvuka malengo ambayo awali ilikuwa tupeleke umeme kwenye vijiji vyote ifikapo mwaka 2025, lakini tutamaliza kazi hii mwezi Juni mwakani.

“Lengo letu ni kuhakikisha tunawafikia watu wote na kuhakikisha huduma ya umeme inapatikana katika vijijini vyote nchini” amesema Mhandisi Olotu.

Aidha Mhandisi Olotu amesema kuwa REA inaendelea kuhamasisha na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini katika maeneo mbalimbali kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara.

Amefafanua kuwa miradi hiyo, ni pamoja na kuongeza wigo wa Gridi ya Taifa kufika kwenye vijiji na vitongoji vyote nchini.

“Tanzania bara kuna vijijini 12,313 na hadi kufikia sasa tayari tumeunganisha umeme katika vijijini 11,313 huku vijiji 1,005 utekelezaji wake unaendelea” amefafanua Mhandisi Olotu.

Ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa mradi wa kupeleka umeme katika vijiji, Serikali imejipanga kufikisha umeme katika vitongoji vyote ili kuhakikisha umeme unafika na kutumika maeneo ya vijijini.

“Serikali kupitia REA ilifanya utambuzi wa wigo wa mradi wa kusambaza umeme katika vitongoji vyote Tanzania Bara.

“Vitongoji ambavyo havijafikiwa na miundombinu ya umeme nchini ni 36,101 kati ya vitongoji 64,790 vilivyopo Tanzania Bara na imegharimu shilingi Trillioni 6.7” ameongeza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile akizungumza kwa niaba ya Wahariri walioudhuria Kakao kazi hicho, ameipongeza Serikali kupitia utendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa hatua kubwa ya kuhakikisha wananchi waliopo vijijini wanafikiwa na umeme, na kwamba kutaongeza kasi ya maendeleo vinijini.

Aidha ametoa mwito kwa Wakala huyo kufanya kazi kwa karibu na vyombo vya habari ili kutoa elimu kwa wananchi na kufahamu namna inavyotekeleza majukumu yake.

Previous articleMHE.KIKWETE: eGA INAJUKUMU NYETI LA KUIHUDUMIA SERIKALI ILI KUTOA HUDUMA KIDIJITALI
Next articleMAJALIWA ATEMA CHECHE MIMBA ZA WATOTO WA SHULE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here