Home BUSINESS PSSSF YATANGAZA FURSA ZA KUPANGISHA KWENYE MAJENGO YAKE MAKUBWA KWA AJILI YA...

PSSSF YATANGAZA FURSA ZA KUPANGISHA KWENYE MAJENGO YAKE MAKUBWA KWA AJILI YA BISHARA, OFISI NA MAKAZI KWENYE MAONESHO YA 7 YA S!TE 2023

NA: K-VIS BLOG, MLIMANI CITY

MAONESHO ya 7 ya Swahili International Expo Tourism (S!TE) 2023,  yaliyoanza Oktoba 6, 2023, kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, yanakamilika leo Oktoba 8, 2023.

Waandaaji wa Maonesho hayo, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) walieleza kuwa lengo la maonesho hayo ni kuwakutanisha wafanyabiashara (wawekezaji) wa hapa nchini, lakini pia wa nje ya nchi. 

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ni mdau mkubwa kwenye uwekezaji na kupitia Maonesho hayo umeshiriki ili kutangaza fursa zinazotokana na uwekezaji wa Mfuko hususan kwenye majengo makubwa ya Biashara na Makazi.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodia ya Utalii Tanzani (TTB), Bw. Damas Mfugale, amesema mwaka huu Serikali inategemea kusaini mikataba itakayowezesha ongezeko kubwa la watalii na wafanyabiashara ya utalii kutoka nje wanaotarajiwa kuja nchini.

Mfuko umewekeza kwenye majengo makubwa ya biashara na makazi, kwenye miji yote mikubwa kama vile Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mtwara na majengo yote hayo yako kwenye maeneo ya kimkakati na yanayofaa kwa shughuli za kiofisi, biashara na hata makazi.

Watumishi wa PSSSF (kulia), wakieleza fursa zinazotokana na uwekezaji wa Mfuko hususan kwenye majengo makubwa ya Biashara na Makazi kwenye miji mikubwa hapa nchini, wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Utalii S!TE ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Previous articleZURA YATANGAZA BEI MPYA ZA MAFUTA ZANZIBAR
Next articleELIMU YA MATUMIZI YA HUDUMA YA PSSSF KIGANJANI YATUA “WAAJIRI HEALTH BONANZA”
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here