Home BUSINESS ZURA YATANGAZA BEI MPYA ZA MAFUTA ZANZIBAR

ZURA YATANGAZA BEI MPYA ZA MAFUTA ZANZIBAR

Na: Halfan Abdulkadir, ZANZIBAR

Mamlaka ya huduma za maji na Nishati Zanzibar ( ZURA) imetangaza bei mpya ya Mafuta huku Dizeli ikipaa Kwa asilimia 9 kutokea Mwezi Septemba Hadi Oktoba mwaka huu.

Taarifa kwa Vyombo vya habari iliyotolewa leo Oktoba 8, 2023 kutoka kitengo Cha Uhusiano cha Mamlaka hiyo imesema Bei ya Petroli Kwa Mwezi huu wa Oktoba Lita 1 itauzwa Shil 3,001 ambapo September ilikuwa ni shil 2,950 ikiwa ni tofauti ya Shil 51.

“Dizeli Mwezi Septemba ilikuwa lita Moja ni Shil 3,012 ambapo kwa mwezi huu wa Oktoba ni Shil 3,282 hii ikiwa ni ongezeko la Shil 270 sawa Asilimia 9” ilisema taarifa hiyo.

Aidha Mafuta ya Taa kwa mwezi Septembana Oktoba imeendelea kusalia katika bei Ile Ile ya Shil 2,921 kwa Lita Moja.

Mafuta ya ndege kwa Mwezi wa September ilikuwa ni Shil 2,448, imepanda Kwa shil ,320 Hivyo Kwa mwezi huu wa Oktoba yanauzwa Kwa Shil 2768 Lita 1.

Sababu za kupanda Kwa Bei hizo za mafuta, ZURA imesema ni kutokana na kuongezeka Kwa bei za Mafuta katika soko la Dunia, gharama za uingizaji wa Mafuta, uwamuzi wa wazalishaji wa Mafuta Duniani (OPEC) kupunguza uzalishaji na vikwazo vya Kiuchumi ambavyo Taifa la Urusi imewekewa na Mataifa ya Magharib.

Bei hizo mpya za Mafuta zitaanza kutumika kuanzia leo Jumapili Oktoba 8, 2023.

Itakumbukwa kwamba Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ( ZURA) imekuwa ikipanga bei za Nishati hiyo kwa kuzingatia mambo mbalimbali yakiwemo Wastani wa mwendeno wa Bei za Mafuta Duniani ( Platts Quotations), Gharama za uingizaji Mafuta katika Bandari ya Dar es salaam na Tanga, Thamani ya Shilingi ya Tanzania kwa Dola za Kimarekani.

Nyingine ni Gharama za usafiri, Bima na ‘Premium’ hadi Zanzibar, Kodi na Tozi za Serikali na Kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

Previous articleDKT. BITEKO APONGEZA CHUO CHA UTALII
Next articlePSSSF YATANGAZA FURSA ZA KUPANGISHA KWENYE MAJENGO YAKE MAKUBWA KWA AJILI YA BISHARA, OFISI NA MAKAZI KWENYE MAONESHO YA 7 YA S!TE 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here