Home BUSINESS DKT. BITEKO APONGEZA CHUO CHA UTALII

DKT. BITEKO APONGEZA CHUO CHA UTALII

Na: Anangisye Mwateba-Dar es salaam

Chuo cha Utalii kimepongezwa kwa kupokea vijana 20 kwa ajili ya kusomea masuala ya Utalii na ukarimu kupitia ufadhili wa Dkt. Samia Suluhu Hassan scholarship.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati , Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko(Mb) wakati akifungua Kongamano la uwekezaji la Wilaya ya Pangani katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Biteko aliweka msisitizo kwa vijana hao 20 ambao wanatoka wilaya ya Pangani kuwa wamepata bahati ya ufadhili huo wakasome kwa nguvu na bidii, pia wajiepushe na mambo maovu ambayo yanaweza kuwaharibia safari yao ya Masomo.

Mhe. Biteko emeipongeza Wizara ya Maliasi na Utalii ikishirikiana na Taasisi zake kwa kuendelea kuzalisha fursa na mazao mapya ya Utalii hasa kwenye Wilaya ambazo zina vivutio vya Utalii.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alisema kuwa kongamano la Utalii la Wilaya ya Pangani litaisaidia wizara kutimiza lengo la kufikia watalii Milioni tano na kufikisha mapato ya Dola za Kimarekani Milioni mia sita ifikapo mwaka 2025.

Previous articleRAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA INDIA
Next articleZURA YATANGAZA BEI MPYA ZA MAFUTA ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here