Home INTERNATIONAL JK ATETA NA KAMATI YA UTATU YA SIASA,ULINZI NA USALAMA (SADC_TROIKA) MJINI...

JK ATETA NA KAMATI YA UTATU YA SIASA,ULINZI NA USALAMA (SADC_TROIKA) MJINI LUANDA_ANGOLA

Na: Mwandishi Wetu, Angola

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, (SADC Panel of Elders) akiwa pamoja na Viongozi wanaounda Kamati ya Utatu ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC- TROIKA) wakijiandaa na Mkutano wa Kamati hiyo unaofanyika leo tarehe 16 Agosti, 2023, Luanda, Angola.

Viongozi hao ni pamoja na Mhe. Hage Geingob, Rais wa Namibia ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa SADC TROIKA, Mhe. Haikande Hichilema wa Zambia ambaye anatarajiwa kuchukua Uenyekiti wa Kamati hiyo na Mhe. Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Kamati hiyo ya SADC TROIKA. Pichani pia ni Mhe. Samuel Matekane, Waziri Mkuu wa Lesotho (wa pili kutoka kulia) na Katibu Mtendaji wa SADC, Mhe. Elias Magosi (wa kwanza kushoto).

Rais Mstaafu Kikwete amewasilisha katika Kamati hiyo ya SADC TROIKA Ripoti ya Kamati ya Uangalizi (Oversight Committee) anayoiongoza katika kufuatilia hatua za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kiasiasa ulipo katika Ufalme wa Lesotho.

Previous articleJUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA TEF YALAANI KUSHABULIWA KWA WAANDISHI WA HABARI NGORONGORO
Next articleWAZIRI MKENDA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA UNICEF TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here