Home INTERNATIONAL BALOZI SHELUKINDO AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA...

BALOZI SHELUKINDO AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE YA INDONESIA

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia Bw. Cecep Herawan katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Pamoja na Mambo mengine, mazungumzo ya viongozi hao yamejikita katika kujadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Indonesia katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na uwekezaji, kilimo, afya, elimu na nishati.

Balozi Shelukindo amemhakikishia Katibu Mkuu huyo ushirikiano wa dhati katika kuendelea kuimarisha uhusiano wa muda mrefu na na Indonesia. Aidha,  amemueleza kwamba mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ni mazuri na salama na kuwasihi wawekezaji kutoka Indonesia kuchangamkia fursa zilizopo.

Naye, Bw. Herawan amepongeza uhusiano imara uliopo baina ya serikali hizi mbili (Tanzania na Indonesia) na kuongeza kuwa Indonesia itaendelea kushirikina na Tanzania katika sekta mbalimbali kwa maslahi ya nchi zote mbili.

Previous articleRAIS SAMIA AMKABIDHI CHETI MUIGIZAJI MAARUFU WA FILAMU NCHINI CHINA JIN DONG KUWA BALOZI WA UTALII NCHINI
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 21-2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here