Home INTERNATIONAL TUTAENDELEA KUKUZA UCHUMI WA AFRIKA – PUTIN

TUTAENDELEA KUKUZA UCHUMI WA AFRIKA – PUTIN

WAZIRI MKUU amesema Serikali ya Urusi imeahidi kushirikiana na Afrika kuboresha uchumi ikiwemo Tanzania.

“Mwelekeo wa mkutano wa leo ilikuwa ni kuona namna gani tunaweza kuboresha uchumi wa nchi za Afrika kwa pamoja na Urusi. Wao wametoa mwelekeo wa namna ambavyo wataweza kushirikiana na nchi za Afrika kuboresha uchumi wa kila nchi na sisi tumeeleza mkakati wa kiuchumi kwenye nchi yetu ambao Rais Putin ameuridhia.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Julai 28, 2023) baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Pili wa Kilele baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na Urusi ambako alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mkutano huo umefanyika kwenye kituo cha mikutano na maonesho cha Expo Forum, jijini St. Petersburg, Urusi. Akizungumza

Waziri Mkuu amesema Tanzania itaendelea kuimarisha miundombinu ya usafirishaji kwa lengo la kuboresha uchumi na biashara kwa kutumia rasilmali zake ikiwemo madini, maliasili na kilimo hasa upatikanaji wa mbolea. “Tumesisitiza pia matumizi ya nishati mbadala kama njia muhimu ya kuwawezesha wananchi wa vijijini ili nao wamudu kutumia nishati mbadala kukuza uchumi wao,” amesema.

Amelitaja eneo jingine kuwa ni kukuza biashara ya mazao baina ya Afrika na Urusi ambapo yenyewe inaweza kuwa soko la moja kwa moja ama kwa kuwatumia marafiki zake. “Ili kufikia hayo, jitihada za kila nchi kwenye kilimo zimesisitizwa. Tanzania tumeeleza mkakati wa kukuza kilimo ikiwemo umwagiliaji. Pia tunahitaji mbolea, madawa na vitendea kazi ili tufanikiwe kwa kasi zaidi.”

Waziri Mkuu aliwaeleza viongozi hao wa Afrika juu ya Mkakati wa Rais Dkt Samia wa kutoa elimu bure na vifaa vya kufundishia kwa lengo la kuwapunguzia mzigo wazazi.

Mapema, akifungua mkutano huo, Rais wa Urusi, Vladmiri Putin alisema nchi za Afrika zimekuwa na mahusiano mazuri na ya muda mrefu na Urusi na kwamba nchi hiyo imekuwa ikiendelea kutoa misaada bila vikwazo kwenye maeneo mbalimbali.

Akitoa mfano, Rais Putin amesema nchi 40 kutoka Afrika zimenufaika na misaada ya kijeshi ikiwemo mafunzo. “Ukaribu wa mahusiano kati ya Afrika na Urusi unazidi kuongezeka. Tunatarajia kufungua balozi zetu kwenye nchi nyingine kama vile Burkina Faso na Equatorial Guinea. Pia tunatarajia kufufua vituo vya utamaduni vya Kirusi. Hivi sasa, vituo kama hivyo vinafanya kazi kwenye nchi nane tu,” alisema.

Alisema nchi hiyo itaendelea kutoa misaada kwenye sekta ya kilimo ili kuimarisha upatikanaji wa chakula. “Jana ndiyo maana nilitoa ahadi ya kuzipatia nafaka nchi sita tani kati ya 25,000 hadi 50,000 na kwamba zitasafirishwa bure.”

Nchi hizo ni Mali, Burkina Faso, Zimbabwe, Jamhuri ya Kati, Eritrea na Somalia. Alisema Urusi imepanga kutoa dola za marekani milioni 90 kwa nchi za Afrika kulingana na maombi ambayo yamepokelewa kutoka Umoja wa Afrika (AU).

Previous articleTAASISI ZA FEDHA ZATAKIWA KUPUNGUZA GHARAMA ZA RIBA YA MIKOPO
Next articleKATIBU MKUU WA CCM NDUGU DANIEL CHONGOLO KUHUTUBIA MAELFU YA WANACCM KAWE JIJINI MKOANI DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here