Home LOCAL WATU WATATU WAFARIKI DUNIA KWA KUZAMA MAJI GEITA.

WATU WATATU WAFARIKI DUNIA KWA KUZAMA MAJI GEITA.

Watu watatu wamefariki dunia na wengine watatu kunusurika katika kijiji cha Nungwe halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani humo kwa kuzama majini ndani ya ziwa Victoria wakati wakivua samaki baada ya chombo chao cha uvuvi (Mtumbwi) kuingiza maji ndani nakusababisha kuzama.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkaguzi wa Jeshi la zima Moto na uokoaji wilaya ya Geita Wambura Fidel amesema wavuvi hao walikuwa sita kwenye chombo cha uvuvi ambapo watatu wamefariki na wengine watatu waliokolewa na wavuvi walio kuwa kalibu baada ya mtumbwi waliokuwa wanatumia kuingiza maji nakusababisha kuzama ndani ya ziwa victoria.

Amesema kutokana na kasi ya maji yaliyokuwa yanaingia kwenye mtumbwi baada ya chombo chao kutoboka yaliwashinda hivyo kupelekea kifo cha wavuvi hao amewataja waliofariki ni David Maliyatabu (25) mkazi wa nugwe, Kamuli Mhoja (20) mkazi wa nungwe na Faustine Cleophance (28) mkazi wa nungwe.

Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe amefika katika eneo la tukio ambapo amewataka wamiliki wa vyombo vya uvuvi (Mitumbwi) kuhakikisha vyombo vyao haviingii majini bila maboya ya kuokolea pamoja na kufanya ukarabati wa mitumbwi hiyo ili kuepuka ajali za majini.

Naye miongoni mwa manusura wa ajali hiyo Dickson Alphonce ameeleza ajali ilivyotokea ambapo amesema mtumbwi waliokuwa wanatumia ulianza kuvuja maji yakaanza kuingia ndani baadae mtumbwi huo ulizama ndipo walipojirusha kwenye maji kila mmoja kwa lengo la kujiokoa.

Previous articleDAWASA WEKENI MIUNDOMBINU YA MAJI KWENYE BUSTANI ZA BARABARANI – RC MAKALLA
Next articleBONNAH AUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA SEKTA MICHEZO JIMBO LA SEGEREA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here