Home LOCAL KATI YA KATA 21 ZA MUSOMA VIJIJINI, 18 ZIMEPAKANA NA ZIWA VICTORIA

KATI YA KATA 21 ZA MUSOMA VIJIJINI, 18 ZIMEPAKANA NA ZIWA VICTORIA

Na : Editha Majura.

KATA 18 kati ya Kata 21 zinazounda Jimbo la Musoma vijijini, zipo kando ya Ziwa Victoria huku shughuli kuu ya wakazi wake ikiwa ni uvuvi.

Hayo yameelezwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sspeter Muhongo, wakati akitoa mchango wake bungeni na kuishauri serikali, hatua za kuchukua ili uvuvi uchangie kikamilifu ukuaji wa uchumi kitaifa.

Alisema tofauti na sasa ambapo uchumi umefikia asilimia 5.6,inatakiwa ukuwe kuanzia kati ya asilimia 8 na Kumi, hali inayoweza kufikiwa kwa kutumia sekta tano, ikiwemo uvuvi.

“Sekta zinazoweza kusababisha uchumi kukua kwa haraka ni Gesi asilia, Madini, Kilimo, Uvuvi na Utalii,” alisema Prof Muhongo.

Alusema kila sekta kati ya hizo kama itachangia uchumi kwa asilimia Mbili, taifa lingekua na uchumi wa kati ya asilimia 8 hadi 10, kabla ya kuweka michango ya sekta nyingine.

Prof Muhongo alishauri sekta ya uvuvi ichukuliwe kibiashara, akirejea mafanikio ya Nchi ya China, ambayo Mwaka jana ilishika nafasi ya kwanza duniani kwa kuzalisha tani 67.5 milioni za Samaki.

Alisema kati ya hizo, tani 54.6 zilizalishwa zilizalishwa kwa kutumia vizimba.

Alishauri serikali Mwaka ujao wa fedha iwekeze zaidi katika sekta hiyo, hususan uvuvi wa vizimba na wananchi wakopeshwe fedha ili wawekeze katika viwanda vya Samaki.

Alisema pamoja na faida nyingine, uvuvi katika vizimba ndiyo suluhisho la kuhadimika Samaki katika Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa na Ziwa Victoria.

Mwisho.

Previous articleWAZIRI MKUU ALITAKA BARAZA LA MICHEZO LA UMOJA WA AFRIKA KUKUZA MICHEZO
Next articleBENKI YA CRDB YAWAHAKIKISHIA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MTAJI WA BIASHARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here