Home LOCAL NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA SHEREHE ZA MEI MOSI-MAJALIWA

NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI KUELEKEA SHEREHE ZA MEI MOSI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na Maandalizi kuelekea sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zitakazofanyika kesho Mei 1, 2023 kitaifa Mkoani Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri.

Ameyasema hayo leo Jumapili (Aprili 30, 2023)alipopokea taarifa na kukagua maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe hizo. Mgeni rasmi atakuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza kamati inayoratibu sherehe hizo na kuwataka kuhakikisha wanakamilisha maeneo ambayo yanahitaji maboresho.

Awali, akitoa taarifa ya maandalizi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Bi. Fatuma Mwasa amesema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tumaini Nyamhokya amesema kwa upande wa vyama vya wafanyakazi maandalizi yamekamilika na wanamatarajio kuwa mahudhurio yatakuwa makubwa na sherehe hizo kuwa za mafanikio.

Previous articleMAKAMU WA RAIS AKISINDIKIZA MWILI WA MTUMISHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Next articleKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA (PIC) YARIDHISHWA NA KASI UENDELEZWAJI MIRADI YA NHC
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here