Home LOCAL SPIKA DKT. TULIA AKIHUTUBIA MKUTANO MKUU WA IPU BAHRAIN

SPIKA DKT. TULIA AKIHUTUBIA MKUTANO MKUU WA IPU BAHRAIN

Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo Machi 12, 2023 amehutubia Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea Nchini Bahrain.

Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Mhe. Ester Matiko ambaye ni Mbunge wa Tanzania anayewakilisha Umoja huo wa IPU wakati wa Mkutano wa 146 unaoendelea Manama Nchini Bahrain.

Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiteta jambo na Mhe. Ester Matiko ambaye ni Mbunge wa Tanzania anayewakilisha Umoja huo wa IPU wakati wa Mkutano wa 146 unaoendelea Manama Nchini Bahrain.

Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kundi la Afrika katika Umoja wa Mabunge Duniani (Africa Geopolitical Group in the IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo Machi 12, 2023 amehutubia Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea Nchini Bahrain wakati Kauli mbiu mkutano huo ni “Kukuza amani na kujenga Jamii Jumuishi yenye kuvumiliana”

Dkt. Tulia amezungumzia kuhusu kuhusu juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Bunge katika kudumisha amani na mahusiano mazuri ya kijamii kwa Wananchi wake pamoja na kuheshimu Maazimio ya Kimataifa katika kulinda na kudumisha amani Duniani.

Wakati huohuo, Dkt. Tulia amewasilisha hoja ya dharura kwa niaba ya kundi hilo kuchagiza kuundwa kwa mfuko wa maafa Duniani kwa ajili ya kusaidia Nchi zinazoathiriwa na majanga ya asili na mabadiliko ya tabianchi.

Pamoja na hoja hii, hoja zingine nne ziliwasilishwa na Mataifa mbalimbali. Hoja hizi zinatarajiwa kupigiwa kura ya maamuzi hapo baadae ili Umoja huo kupitisha hoja moja ya dharura ambayo itajadiliwa, kuboreshwa na hatimaye kutengeneza azimio la Mkutano huo.

Previous articleMAKAMU WA RAIS AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKUU WA WILAYA
Next articleTANZANIA NA AFRIKA KUSINI KUONGEZA MAENEO MAPYA YA USHIRIKIANO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here