Home LOCAL Cde: MBETO: ASISITIZA VYOMBO VYA HABARI KUTOA TAARIFA SAHIHI

Cde: MBETO: ASISITIZA VYOMBO VYA HABARI KUTOA TAARIFA SAHIHI

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg.Kamis Mbeto Khamis (kushoto),akizingumza na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC),Salum Ramadhan Abdallah (kulia), katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya Habari vilivyopo Zanzibar.leo tarehe 20/03/2023.

NA: IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Khamis Mbeto Khamis, amevisihi vyombo vya habari  nchini kuongeza kasi ya utoaji wa taarifa sahihi na zilizofanyiwa utafti wa kina unakidhi vigezo vya taaluma za uandishi wa habari.

Rai hiyo ameitoa kwa wakati tofauti katika mwendelezo wa ziara zake katika vyombo vya habari Zanzibar,alisema vyombo vya habari ni wadau muhimu katika kuhabarisha,kuelimisha na kutangaza fursa mbalimbali za maendeleo katika nyanja za kiuchumi,kisiasa na kijamii.

Mbeto,alisema taarifa sahihi zinazotolewa katika vyombo vya habari ni kiunganishi muhimu cha wananchi kujua kuhusu kazi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi.

Alifafanua kuwa ni vyema vyombo hivyo vikaendelea kutoa taarifa za matukio mbalimbali yanayofanywa na viongozi wakuu ili yawafikie wakaazi wa maeneo mbalimbali hususani vijijini.

Katika maelezo yake, Katibu huyo wa Kamati Maalum, alieleza kuwa serikali imekuwa ikifanya shughuli mbalimbali ambazo vyombo vya habari vinastahili kuvitangaza kwa lengo la kuhabarisha wananchi.

“Nimekutembeleeni kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina yenu na Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, kwani bila nyinyi hakuna shughuli za kisiasa zinazoweza kufanyika nchini.

Najua thamani na nguvu ya vyombo vya habari nchini na duniani kote,naahidi kukupeni ushirikiano na kipaumbe kwa kila jambo litakalotokea CCM.”alisema Mbeto.

Sambamba na hayo, alivitaka vyombo vya habari kuhakikisha taarifa zinazotoa hazichochei uvunjifu wa amani.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar(ZBC) Salum Ramadhan,alisema vyombo vyombo vya habari vinavyomilikiwa na shirika hilo vimekuwa na watizamaji na wasikilizaji wengi kutokana na kuwa na vipindi bora vya kijamii.

Salum, alisema shirika hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za upungufu wa vitendea kazi na huduma za usafiri kwa watendaji wa shirika hilo wanaoingia zamu za wakati wa usiku.

Alisema uongozi wa Shirika hilo lipo tayari kushirikiana na CCM katika kuitangaza matukio ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025.

Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa shirika la magazeti ya Serikali,Ali Haji Mwadini,alieleza kuwa pamoja na mafanikio yaliyofikiwa katika taasisi hiyo bado wanakabiliwa na changamoto ya ofisi ya shirika hilo kuwa ndogo ambayo haikidhi mahitaji yao.

Akizitaja changamoto nyengine, Mwadini alisema ni pamoja na uhaba wa wafanyakazi katika Gazeti la kiingereza ambapo alisema kuna ulazima kutumia watu kutoka nje ya shirika hilo.

“Zaidi ya asilimia 80 ya mapato yanayopatikana kutokana na uzalishaji yanakwenda kwenye uchapishaji kutokana na shirika halina mtambo wa kuchapishia magazeti,”alisema.

Hivyo, aliahidi kuendelea kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi katika utekelezaji wa Ilani sambamba na kuahidi kuendelea kutangaza maendeleo yanayopatikana.

Kwa upande wao wamiliki wa vyombo vya Habari binafsi vikiwemo vya RVS TV (Online),Mjini FM na Adhana FM walisema vyombo vyao havina ruzuku kutoka serikalini hivyo wanakabiliwa na upungufu wa fedha za uendeshaji kutokana na kutegemea matangazo ya serikali na makampuni binafsi.

Katibu Mbeto alifanya ziara katika vyombo vya habari, ikiwemo Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Shirika la Magazeti ya Serikali ya Zanzibar (Zanzibar Leo), RVS, Adhana FM na Mjini FM.

Previous articleBANDARI KAVU YA KWALA KUANZA KUTOA HUDUMA HIVI KARIBUNI
Next articleBENKI YA CRDB, SILENT OCEAN ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUWASAIDIA WAFANYABIASHARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here