Home INTERNATIONAL WAZIRI TAX APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WA MISRI,...

WAZIRI TAX APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WA MISRI, MAREKANI

 

Dar es Salaam, 10 Februari 2023
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amepokea nakala za Hati za Utambulisho za mabalozi wateule wa nchi za Misri na Marekani.

Mhe. Waziri Tax amepokea nakala za hati za utambulisho za Balozi wa Misri nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail na Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Michael Battle jana jioni katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti mara baada ya kupokea nakala zao za hati za utambulisho, Dkt. Tax amewahakikishia ushirikiano kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao hapa nchini na kuwasihi kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na nchi zao.

Balozi mteule wa Misri nchini, Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail ameahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Misri na Tanzania katika sekta za nishati hususani mradi wa bwawa la mwalimu Nyerere, kilimo, biashara na uwekezaji.

“Misri na Tanzania tunayo mengi ya kushirikiana, tunaahidi kuendeleza ushirikiano wetu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili, wakati wa utumishi wangu hapa Tanzania nitaendeleza kwa maslahi mapana ya wananchi wetu wote,” alisema Balozi Ismail.

Kwa upande wake Balozi Mteule wa Marekani, Mhe. Michael Battle amesema Marekani na Tanzania zimekuwa marafiki wa muda mrefu, na itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta za Utalii, Kilimo, afya, biashara na uwekezaji pamoja na sekta nyingine za kimkakati.

“Ni furaha kwangu kuwepo hapa leo na kukabidhi nakala ya hati ya utambulisho wangu hapa nchini Tanzania, napenda kuahidi kwa kipindi nitakachokuwa hapa nitahakikisha kuwa uhusiano wetu wa kidiplomasia unakuwa na kuimarika kwa maslahi ya mataifa yetu,” alisema Balozi Battle.

Previous articleHALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM YAPITISHA BAJETI SH. BILIONI 90
Next articleZAO LA MPIRA KUENDELEZWA MAENEO YENYE HALI  YA HEWA INAUYOKUBALIKA NCHINI 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here