Home SPORTS SAIDOO ATUA SIMBA RASMI

SAIDOO ATUA SIMBA RASMI

Mshambuliaji raia wa Burundi, Saido Ntibazonkiza rasmi amesajiliwa na Simba SC kwa kandarasi ya mwaka mmoja na nusu akitokea katika Klabu ya Geita Gold ya mjini Geita ambapo alisajiliwa kwa mkataba wa mwaka mmoja pekee akitokea Yanga SC.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba SC, imeeleza kuwa Uongozi wa Klabu hiyo umefika makubaliano ya kumsajili mchezaji huyo mwenye uzoefu mkubwa akiwa amecheza Ligi mbalimbali ulimwenguni katika nchi za Ufaransa, Uturuki, Poland na Tanzania kwa zaidi ya misimu miwili.

Ntibazonkiza akiwa na Geita Gold FC alipachika wavuni mabao manne akitoa ‘assist’ sita, tayari amewasili jijini Mwanza kujiunga na Kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi ambacho kinajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara dhidi ya KMC FC utakaopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba, Desemba 26 mwaka huu.

Usajili wa Ntibazonkiza unakuwa wa kwanza kwa Kikosi cha Simba SC katika dirisha dogo la usajili, huku Wekundu hao wa Msimbazi wakitoa taarifa ya kufanya usajili wao kwa umakini bila shinikizo kutoka mahali popote.

Previous articleMAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DISEMBA 24 -2022
Next articleRC MTAKA AKABIDHI ZAWADI ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KWA NIABA YA RAIS SAMIA WANG’ING’OMBE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here