Home LOCAL RC MTAKA AKABIDHI ZAWADI ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KWA NIABA YA...

RC MTAKA AKABIDHI ZAWADI ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KWA NIABA YA RAIS SAMIA WANG’ING’OMBE

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ametoa wito kwa watanzania wanaorudi nyumbani kwao kwa ajili sikuku za mwisho wa mwaka,kwenda kutoa sadaka za shukrani kuliko kuishia kufanya sherehe kubwa au kukesha sehemu za starehe kwa kufurahia kuvuka mwaka.
Mtaka ametoa wito huo wakati akikabidhi sadaka ya mwisho wa mwaka kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan katika kituo cha kulea watoto yatima cha Renato Glandi kinachomilikiwa na jimbo Katoliki la Njombe na kusimamiwa na Parokia ya Ilembula wilayani Wanging’ombe.
“Mnaotoka kwenye eneo moja kwenda nyumbani kwenu kwamba mnaenda kusheherekea mwisho wa mwaka,msiishie tu kula nyama na kukesha baa,mkashiriki sehemu ya kile mlichokipata kwa mwaka huu kugusa kundi fulani ili hata kesho ukifika safari yako ya mwisho duniani kiongozi wako wa kiroho apate cha kukuhubiria” Amesema Mtaka
Miongoni mwa Sadaka iliyotolewa na Rais Dkt,Samia mkoani Njombe katika kituo hicho kwa niaba ya vituo vingine vya mkoa huo ni pamoja na Mchele 100KG,Maharage 50KG,Katoni 16 za Soda na Mbuzi wanne.
Previous articleSAIDOO ATUA SIMBA RASMI
Next articleWAZIRI MKUU AAGIZA WAKUU WA WILAYA KUKUTANA NA WAFUGAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here