Home LOCAL KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AFUNGA OFISI DAR ILI VIONGOZI WATII AGIZO...

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AFUNGA OFISI DAR ILI VIONGOZI WATII AGIZO LA KUHAMIA DODOMA

Na. WAF- Dar es Salaam, 23/12/2022

Menejimenti ya Wizara ya Afya chini ya Katibu Mkuu Prof. Abel Makubi imechukua hatua za kuifunga Ofisi ya Uratibu wa Miradi wa Ukimwi, TB na Malaria (COAg) iliyopo chini ya Wizara ya Afya ambayo inasimamiwa na Dr Peter Mgosha kwa kukaidi agizo la Rais na Waziri Mkuu kuhamia makao makuu Dodoma.

Prof. Makubi amebainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Dkt. Mgosha amekaidi zaidi ya mara tatu agizo la kuhamia Dodoma pamoja na kukumbushwa na Menejimenti ya Wizara.

Katibu Mkuu ameagiza watumishi wote wa ofisi hiyo wafike Dodoma Jumatatu bila kukosa.

Menejimenti imechukua hatua ya kufunga ofisi hiyo na hatua zingine za kinidhamu ziendelee chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu.

Previous articleMAKUMBUSHO YA TAIFA YAWAAGA WASTAAFU
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DISEMBA 24 -2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here