Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Chuo cha UAUT Mchungaji Stanley Mndasha akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la ibada katika Chuo hicho.
Naye Mkuu wa Idara ya Biashara wa Chuo hicho Nelson Omar Rahul akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT) Kilichopo Kigamboni Profesa Ho Chan Hwang (kushoto) akifurahia jambo na mmoja wa watumishi wa Chuo hicho katika hafla hiyo iliyofanyika Leo Disemba 11,2022 katika Chuo hicho, Kigamboni Dar es Salaam.
Watumishi wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo hicho katika hafla hiyo.
Taasisi za Elimu nchini vikiwemo Vyuo vikuu nchini vimetakiwa kumtanguliza Mungu katika masuala mbalimbali ya Kitaaluma na Tafiti ili yaweze kuleta manufaa kwa Jamii na Taifa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT) Kilichopo Kigamboni Profesa Ho Chan Hwang wakati wa uzinduzi wa Jengo la Ibada lililopo Chuoni hapo kwa lengo la kumuabudu Mungu kabla na baada ya masomo ambapo amesema watu kuwa na hofu ya Mungu kutachochea uwepo wa Amani.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Chuo cha UAUT Mchungaji Stanley Mndasha amesema matukio ya mauaji na ukatili unaoripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini unatokana na ukosefu wa mafundisho ya neno la Mungu, hivyo kupitia chuo hicho wanajikita kufundisha umuhimu wa suala hilo, ambalo ni mchango mkubwa katika kuchangia kupinga ukatili wa kijinsia.
Naye Mkuu wa Idara ya Biashara wa Chuo hicho Nelson Omar Rahul amesema elimu inayotolewa na Chuo imejikita zaidi kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizopo na pia kinatoa ufadhili wa wanafunzi nje ya nchi.