Home LOCAL CHUO KIKUU CHA UMOJA WA AFRIKA (UAUT) CHAZINDUA JENGO JIPYA LA IBADA

CHUO KIKUU CHA UMOJA WA AFRIKA (UAUT) CHAZINDUA JENGO JIPYA LA IBADA

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Chuo cha UAUT Mchungaji Stanley Mndasha akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la ibada katika Chuo hicho.

Naye Mkuu wa Idara ya Biashara wa Chuo hicho Nelson Omar Rahul akizungumza katika hafla hiyo.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT) Kilichopo Kigamboni Profesa Ho Chan Hwang (kushoto) akifurahia jambo na mmoja wa watumishi wa Chuo hicho katika hafla hiyo iliyofanyika Leo Disemba 11,2022 katika Chuo hicho, Kigamboni Dar es Salaam.

Watumishi wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Chuo hicho katika hafla hiyo.

Taasisi za Elimu nchini vikiwemo Vyuo vikuu nchini vimetakiwa kumtanguliza Mungu katika masuala mbalimbali ya Kitaaluma na Tafiti ili yaweze kuleta manufaa kwa Jamii na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT) Kilichopo Kigamboni Profesa Ho Chan Hwang wakati wa uzinduzi wa Jengo la Ibada lililopo Chuoni hapo kwa lengo la kumuabudu Mungu kabla na baada ya masomo ambapo amesema watu kuwa na hofu ya Mungu kutachochea uwepo wa Amani.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Chuo cha UAUT Mchungaji Stanley Mndasha amesema matukio ya mauaji na ukatili unaoripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini unatokana na ukosefu wa mafundisho ya neno la Mungu, hivyo kupitia chuo hicho wanajikita kufundisha umuhimu wa suala hilo, ambalo ni mchango mkubwa katika kuchangia kupinga ukatili wa kijinsia.

Naye Mkuu wa Idara ya Biashara wa Chuo hicho Nelson Omar Rahul  amesema elimu inayotolewa na Chuo imejikita zaidi kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizopo na pia kinatoa ufadhili wa wanafunzi nje ya nchi.

Previous articleWANAFUNZI WA SHULE ZA MSALALA WAPATIWA ELIMU YA KUJITAMBUA NA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA KUPITIA PROGRAM YA BARRICK BULYANHULU
Next articleMJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM HEMEDI SULEIMAN ABDULLA ASHIRIKI MAPOKEZI YA DKT. MWINYI ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here