Home LOCAL UNHCR TANZANIA IMEFANIKIWA 

UNHCR TANZANIA IMEFANIKIWA 

AFISA Muhifadhi Wakimbizi Mwandamizi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), nchini Tanzania Boniface Kinyanjui amesema, Serikali ya Tanzania imefanikiwa kulinda amani yake.

Kinyanjui alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye warsha ya siku tatu na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2022.

‘‘Amani haitoki juu kushuka chini, inalindwa na serikali, Serikali ya Tanzania imefanikiwa katika hili.…, Tanzania ni nchi ya amani lakini imezingirwa (na nchi zenye wasiwasi wa amani),’’ alisema.

Ofisa huyo alisema, Tanzania ni nchi iliyohifadhi wakimbizi kwa muda mrefu tangu uhuru na kwamba, ni miongini mwa nchi chache mabazo ziliruhusu baadhi ya wakimbizi kuwa raia wake.

‘‘Tanzania imepokea wakimbizi kutoka Ulaya, Marekani n ahata Kenya hapo. Ni miongoni mwa nchi chache zilizowapa wakimbizi uraia wan chi yake,’’ alisema.

Hata hivyo alisema, UNHCR hupenda zaidi zaidi kuona walimbizi wakipewa hifadhi pamoja na ruhusa ya kuendelea na maisha yao ya uzalishaji mali na si kuwekwa pamoja kwenye makambi.

‘‘Wakimbizi na watu wanaoomba hifadhi sio watu wanaopendwa sana katika nchi nyingi. Sisi tungependa kuona wakimbizi wakipewa nafasi ya kujimudu kimaisha katika uzalishaji mali maana ni wanadamu kama wengine.

‘‘Katika wakimbizi kuna wataalamu wengi ambao wanaweza kusaidia jamii. Mfano; kuna mkimbizi alitoka Sudani Kusini na lipita Tanzania akaenda Afrika Kusini. Huko yey ndiye aliyetengeneza mfumo wa kuingiza hewa kwenye mwili kupitia tundu za pua wakati ule wa UVIKO-19,’’ alisema.

Akizungumzia shirika hilo, Kinyanjui aliema UNHCR ilianzishwa mwaka 1950 na kwamba, mwaka 1951 ndio ilianza kuingia mikataba ya amani

‘‘Lengo kubwa la UNHCR ni kulinda haki ya mfungwa na mahitaji yake kokote atakapokuwa,’’ alisema.

Previous articleUVCCM KISUTU WATOA MSAADA PHOTOCOPY MASHINE
Next articleTRA SHINYANGA YAZINDUA WIKI YA SHUKRANI KWA MLIPA KODI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here