Home LOCAL ENG MLAVI- UJENZI WA BARABARA YA SONGEA BYPASS KUHARAKISHA MAENDELEO YA MKOA...

ENG MLAVI- UJENZI WA BARABARA YA SONGEA BYPASS KUHARAKISHA MAENDELEO YA MKOA WA RUVUMA

Meneja wa wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS)Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi kulia akikagua eneo linalotarajia kupita Barabara ya mchepuko(Songea Bypass)Changarawe Manispaa ya Songea ambayo  ujenzi wake utaanza hivi karibuni,kushoto ni Mhandisi wa mipango wa TANROADS Rubara Marando wa  na Mhandisi Izak Issa kutoka ofisi ya meneja wa TANROADS mkoa wa Ruvuma.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS)mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi kulia, akimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya Nenda kwa Usalama Barabarani wilaya ya Songea Pascal Msigwa wa kushoto na Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Ruvuma(Ruvuma Press Club)Andrew Chatwanga katikati, walipotembelea eneo la Msamala ambapo kutajengwa Barabara ya mzunguko(Round about)itakayounganisha Barabara kuu ya Songea-Njombe na Barabara ya mchepuko ya Songea Bypass inayotarajia kuanza ujenzi wake hivi karibuni.

 

Baadhi ya nyumba zinazotakiwa kuvunjwa katika mtaa wa Namanditi Manispaa ya Songea ili kupisha  ujenzi wa mradi wa Barabara ya Mchepuko kutoka Namanditi hadi Changarawe  inayotarajia kuanza ujenzi wake hivi karibuni.

Mkazi wa  mtaa wa Namanditi Manispaa ya Songea Mariam Mwele kulia ambaye nyumba yake italazimika kuvunjwa ili kupisha ujenzi wa mradi wa Barabara ya Mchepuko(Songea ByPass) yenye urefu wa km 14.3 akizungumza na mwakilishi wa Kituo cha Itv na Radio One mkoani Ruvuma Emmanuel Msigwa ambapo ameiomba Serikali kuwalipa fidia  haraka wananchi watakaovunja nyumba zao ili kupisha ujenzi wa mradi huo.

Picha zote na Muhidin Amri,

Na: Muhidin Amri, Songea

WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Ruvuma, iko katika hatua ya mwisho kuanza  ujenzi wa Barabara ya  mchepuko ( Songea ByPass) maarufu kama (Mtwara Corridor)yenye urefu wa km 14.3.

Meneja wa TANROADS mkoani Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi alisema,barabara hiyo ni sehemu ya ujenzi wa mradi wa Barabara kuu ya Songea-Makambako.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mlavi ni kwamba,ujenzi wa Barabara hiyo itaanzia eneo la Namanditi ambapo itapita kata ya Mwenge msindo,Msamala, kituo cha kupoza umeme  Unangwa hadi  Changarawe Barabara kuu ya Songea-Tunduru.

Aidha alisema,katika mradi huo kutakuwa na eneo la mzunguko (round about) tatu  ya kwanza itejengwa eneo la Namanditi,ya pili Msamala karibu na kituo cha mafuta cha Ottawa na nyingine itajengwa eneo la Changarawe Barabara kuu ya Songea-Tunduru.

Alisema, pindi Barabara hiyo itakapojengwa itasaidia sana kuondoa changamoto ya msongamano wa magari katikati ya mji wa Songea hasa malori yanayobeba makaa ya mawe na itakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi.

“Barabara  hii ya mchepuko(Songea Bypass) ina umuhimu mkubwa na itaongeza fursa nyingi  za kiuchumi kwa wakazi  wa mkoa wa Ruvuma  na wale wanaofika kutoka mikoa mingine ya  jirani”alisema Mlavi.

Kwa mujibu wa Mlavi, tathimini ya fidia kwa ajili ya kuwalipa wananchi  watakaopitiwa na  mradi huo imeshafanyika  na sasa Serikali iko katika hatua ya mwisho ya malipo ili wananchi waweze kupisha ujenzi wa mradi huo.

Mhandisi Mlavi, amewataka wananchi wa mkoa wa Ruvuma na Watanzania kwa ujumla kuiamini Serikali yao kwani imejipanga vyema kwa ajili ya kutekeleza mradi huo na miradi mingine katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma.

“nachukua nafasi hii kuwatoa wasiwasi wananchi kuhusu ujenzi wa Barabara hii kwani serikali iko kazini na imejipanga kuhakikisha  itajengwa kwa kama ilivyokusudia”alisema Mlavi.

Naye Mhandisi Izaki Issa kutoka ofisi ya meneja wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS)mkoa wa Ruvuma alisema, Barabara  hiyo ya mchepuko itapita katika vijiji vitano vya Namanditi,Luwawasi,Mtaungana,Osterbay na Kuchile.

Baadhi ya wananchi,wameiomba Serikali kuanza ujenzi wa Barabara hiyo  haraka ili iweze kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Ruvuma na kuharakisha maendeleo yao.

Mariam Mwela mkazi wa Namanditi alisema, wameupokea mradi huo kwa mikono miwili kutokana na faida zake kiuchumi  na ameipongeza TANROADS mkoa wa Ruvuma kufikiria kujenga Barabara  ya mchepuko katika mji wa Songea.

Aidha,ameiomba Serikali kuwalipa fidia zao mapema ili wakatafute maeneo mengine  ya kuishi,kwani tangu TANROADS ilipoweka alama za X kwenye nyumba zao wanashindwa kuendeleza maeneo yao na wanaishi kwa hofu kubwa.

Pascal Msigwa(Top One)alisema,mradi huo ni muhimu sana kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma na kuipongea serikali ya awamu ya sita kwa kuonyesha nia ya kujenga  Barabara hiyo na  Barabara kuu ya Songea-Makambako.

Rajabu Kanganya mwendesha bodaboda, ameiomba Serikali kupitia TANROADS mkoa wa Ruvuma,kuhakikisha mradi huo unaanza haraka badala ya kuchukua muda mrefu.
MWISHOOOO.

Previous articleKIDUKU AIBUKA MBABE DHIDI YA KHALED
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 26-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here