Home LOCAL EWURA YAKUTANA NA WAHARIRI WA HABARI KATIKA KIKAO KAZI JIJINI DAR

EWURA YAKUTANA NA WAHARIRI WA HABARI KATIKA KIKAO KAZI JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Modestus Lumato (kulia aliyesimama) akizungumza katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika leo Julai 16,2022 Jijini Dar es Salaam kilicholenga kufahamiana na kubadirishana mawazo kwa pamoja ambapo pia Mkurugenz huyo amezungumzia matumizi ya Gesi kwenye magari na majumbani na kupanda kwa Bei ya mafuta. (kushoto aliyekaa) ni Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile (kushoto aliyekaa) akipiga makofi kupongeza hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Modestus (kulia anaezungumza) wakati alipokuwa akizungumza katika Kikaokazi hicho.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile  (kushoto aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano huo.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA Titus Kaguo akizungumza kwenye kikao hicho alipokuwa akiwakaririsha wahariri wa vyombo vya habari (hawamo pichani) kwenye kikao hicho kilichofanyika leo Julai 16,2022 Jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi Huduma kwa wateja wa EWURA Kanda ya Mashariki Getrude Mbiling’i akifuatilia mkutano huo.

Na: Thobiesa Makafu.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo Tar.16/07/2022, imekutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari chini ya  Jukwaa la Wahariri (TEF) nchini ili kujadili masuala mbalimbali kuhusu udhibiti wa huduma za nishati na maji.
Akifungua Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha. Modestus Lumato alisema, “wahariri wa vyombo vya habari wana jukumu muhimu sana katika kuhabarisha jamii, hivyo mkutano huu unalenga kujadiliana na kuongeza uelewa juu ya sekta zinazodhibitiwa pamoja na kupokea maoni na ufafanuzi juu ya masuala ya kiudhibiti”.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Bw. Deodatus Balile ameeleza, wahariri wataendelea kushirikiana na EWURA katika utekelezaji wa shughuli za udhibiti kwa maslahi mapana ya watanzania.
“EWURA inathamini mchango wa tasnia yetu ya habari, nasi tunaahidi kuendelea kutoa ushirikiano  kila wakati”
Akitoa neno la shukrani, Mwandishi mkongwe Salim Salim ameeleza kuwa, kazi zinazofanywa na wahariri pamoja na waandishi wa habari nchini, ni utekelezaji wa wajibu wao hivyo watatumia nafasi walizonazo kuhakikisha wananchi wanaelewa masuala ya udhibiti wa huduma za nishati na maji.

BAADHI YA WAHARIRI WA HABARI WAKIFUATILIA MKUTANO HUO.

Previous articleWANANCHI WA KIJIJI CHA ANGALIA WAISHUKURU SERIKALI KUFIKISHA HUDUMA YA UCHUNGUZI WA KIFUA KIKUU
Next articleMWANRI AIPONGEZA SERIKALI KUONGEZA MSULI SEKTA YA KILIMO…ATAKA KUZALISHA VYA ZIADA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here