Na: Costantine James, Geita.
Klabu ya Geita Gold Fc Yenye masikani yake mkoani Geita imetembelea uwanja wao unaondelea kujengwa Magogo wilayani Geita na kujionea hali halisi ya ujenzi wa uwanja huo.
Maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo yanaendelea vizuri ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 95% Mhandisi Juma Nyajawa kwa kushirikiana na kampuni ya GGMl ambao ndio wadhamini wakuu wa timu hiyo amesema mpaka sasa uwanja huo unaendelea vizuri.
Mhandisi Nyajawa amesema kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo utachukua kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa kwani changamoto waliyokuwa nayo tayari imekwisha kutatuliwa hivyo wanaendelea na ujenzi.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka kampuni ya uchimbaji dhahabu (GGML) ambaye pia ni Meneja Mwandamizi kitengo cha Ushirikiano Bw.Manace Ndoroma amesema wameridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa uwanja huo.
Manace Amesema mpaka sasa GGML imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.4 kwa mkandarasi anayetekeleza ujenzi huo.
Amesema wao kama GGML watahakikisha wanashirikiana na halmashauri ya mji Geita ili kuweza kuhakikisha ujenzi wa uwanja huo unakamilika kwa wakati na kuiwezesha timu ya Geita Gold Fc kuanza kuutumia uwanja huo kama uwanja wao wa nyumbani.
Ikumbukwe kuwa timu ya Geita Gold Fc ipo katika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa inafanya vizuri kwenye michezo yake ndani ya Ligi kuu Tanzania bara.