Home SPORTS UJENZI WA UWANJA WA GEITA GOLD FC WAFIKIA ASILIMIA 80.

UJENZI WA UWANJA WA GEITA GOLD FC WAFIKIA ASILIMIA 80.

Na: Costantine James, Geita.

Klabu ya Geita Gold Fc Yenye masikani yake mkoani  Geita imetembelea uwanja wao unaondelea kujengwa Magogo wilayani Geita na kujionea hali halisi ya ujenzi wa uwanja huo.

Maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo yanaendelea vizuri ambapo mpaka sasa umefikia   asilimia 95% Mhandisi Juma Nyajawa kwa kushirikiana na kampuni ya GGMl ambao ndio wadhamini wakuu wa timu hiyo amesema mpaka sasa uwanja huo unaendelea  vizuri.

Mhandisi Nyajawa amesema  kukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo utachukua kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa kwani changamoto waliyokuwa nayo tayari imekwisha kutatuliwa hivyo wanaendelea na ujenzi.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka  kampuni ya uchimbaji dhahabu (GGML) ambaye pia ni Meneja Mwandamizi kitengo cha Ushirikiano Bw.Manace Ndoroma amesema wameridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa uwanja huo.

Manace Amesema mpaka sasa  GGML imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.4 kwa mkandarasi anayetekeleza ujenzi huo.

Amesema wao kama GGML  watahakikisha wanashirikiana na halmashauri ya mji Geita ili kuweza  kuhakikisha  ujenzi  wa uwanja huo unakamilika kwa wakati na kuiwezesha timu ya Geita Gold Fc kuanza  kuutumia uwanja huo kama uwanja wao wa nyumbani.

Ikumbukwe kuwa timu ya Geita Gold Fc ipo katika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara ikiwa inafanya vizuri kwenye michezo yake ndani ya Ligi kuu Tanzania bara.

Previous articlePOLISI YAIFUATA NAMUNGO LEO
Next articleKMC FC WAPO FITI KUIVAA PRISONS KESHO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here