Home SPORTS POLISI YAIFUATA NAMUNGO LEO

POLISI YAIFUATA NAMUNGO LEO

Na: Stella Kessy.

JUMLA ya wachezaji 20 wa timu ya Polisi Tanzania pamoja na viongozi 7 wa benchi la ufundi wameifuata Namungo katika mchezo utakaochezwa Juni 16.

Akizungumza na blog hii ya Green waves media kuelekea mchezo huo msemaji wa timu hiyo Hassan Juma amesema kuwa kikosi kimejiandaa vyema kwa kupambana na kupata MATOKEO katika mchezo huo.

“Sina shaka na kikosi changu kwani tumepata muda wa kufanyia kazi mapungufu hivyo kikosi Kwa sasa kipo imara kwa kupambana na kuondoka na alama 3 ugenini kikubwa wadau na wapenzi wa timu wazidi kuiombea” amesema.

Ameongeza kuwa baadhi ya wachezaji watano wamebaki kambini Dar es Salaam na wataungana na wenzao wakirejea Lindi kwa mchezo dhidi ya Yanga Jun 22 uwanja wa Mkapa.
Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO JUMATATU JUNI 13-2022
Next articleUJENZI WA UWANJA WA GEITA GOLD FC WAFIKIA ASILIMIA 80.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here