Home SPORTS KMC FC WAPO FITI KUIVAA PRISONS KESHO

KMC FC WAPO FITI KUIVAA PRISONS KESHO

Na: Stella Kessy.

UONGOZI wa  KMC FC umesema kuwa wamejipangab vyema katika mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons  utakaochezwa kesho katika dimba la Uhuru.

Akizungumza na blog hii afisa Habari na Mawasiliano KMC FC  Christina Mwagala wachezaji wote wapo tayari kwa mtanange huo.

Amesema kuwa katika kipindi chote ambacho timu zilikuwa kwenye mapumziko, KMC iliingia kambini Mei 27 na kuanza program mbalimbali ambapo zimefanyika kwa ufanisi mkubwa ikiwemo kucheza mechi za kirafiki na kwamba hadi sasa Ligi inarejea kila mmoja anafahamu umuhimu wa mchezo huo licha ya kwamba utakuwa na ushindani kutokana na kila Timu kuhitaji matokeo.

“Tunakwenda kwenye mechi ngumu na bora, tunafahamu Prisons ni wazuri wanajipanga wasipoteze, lakini kwa upande wa KMC tunajua ubora wa wachezaji wetu tulionao pamoja na benchi la ufundi hivyo tunahitaji kutumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani kuzipata alama tatu.

“Ligi hivi sasa inakwenda ukingoni na kila mtu anahitaji kutetea nafasi ya kuendelea kuwepo katika msimu ujao, ndio mana tunafahamu ugumu wa mchezo wa kesho, lakini mashabiki wasihofu, timu imeandaliwa vizuri na kwamba wajitokeze kutoa sapoti ili kuongeza morali zaidi kwa wachezaji.

Previous articleUJENZI WA UWANJA WA GEITA GOLD FC WAFIKIA ASILIMIA 80.
Next articleBODI YA WANAHABARI ISIMAMIWE NA WANAHABARI – AG FELESHI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here