Home BUSINESS ANZANIA COMMERCIAL BANKI YATANGAZA KUPATA FAIDA YA BILIONI 19.7

ANZANIA COMMERCIAL BANKI YATANGAZA KUPATA FAIDA YA BILIONI 19.7

Mwenyekiti wabodiya Tanzania Commercial Bank Dkt. Edmund Mndolwa (katikati), akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kupata faida ya shilingi Bilioni 19.7 kwa mwaka ulioishia Desemba 31 2021 hatua inayo tajwa kuwa yamafanikio na kuimarika kwa benki hiyo ambayo ni muunganiko wa iliyokuwa benki ya TPB na TIB Corparate.

Afisa MtendajiMkuuwa Tanzania Commercial Bank TCB, Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa hafla ya kutangaza faida ya shilingi Bilioni 19.7 kwa mwaka ulioishia Desemba 31 2021 hatua inayotajwa kuwa ya mafanikio na kuimarika kwa benki hiyo ambayo ni muunganiko wa iliyokuwa benki ya TPB na TIB Corparate.

 Mwenyekitiwabodiya Tanzania Commercial Bank Dkt. Edmund Mndolwa (katikati), akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kupatafaida ya shilingi Bilioni 19.7 iliyopata benki hiyo wa pilikulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB, Sabasaba Moshingi pamoja na maafisa wengine wa benki hiyo 

Tanzania Commercial Bank TCB imetangaza kupata faida ya shilingi Bilioni 19.7 kwa mwakaulioishiaDesemba 31 2021 hatua inayotajwa kuwa ya mafanikio na kuimarika kwa benki hiyo ambayo ni muunganiko wa iliyokuwa benki ya TPB na TIB Corparate.

Mwenyekitiwabodiya Tanzania Commercial Bank Dkt. Edmund Mndolwa ametoa taarifahiyo katika mkutano wa mwaka wa wanahisa wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar esSalaam  nakusema kuwa faida hiyo ni kabla ya kodi.

Faida iliyopatikana mwaka 2021 inatajwa na uongozi wa benki kuwa ni kubwa kufuatia ile ya mwaka 2020 ambayo haijawahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwa Benki ya TCB takriban miaka 95 iliyopita

Amepongeza uongozi pamoja na wafanyakazi wa Tanzania Commercial Bank kwakuchangia mafanikio hayo licha ya changamoto zamdororo wauchumi uliosababishwa na wimbi la ugonjwawa UVOKO-19  ambao pia umeathiri uchumi wamataifa mengi duniani.

Kwaupande wake Afisa Mtendaji Mkuuwa Tanzania Commercial Bank TCB, Sabasaba Moshingi amesema kufuatia mafanikio hayo,wanahisa wamekubaliana kutoa gawio la hisa na kuelekeza   kwenye kuimarisha mtajiwa Benki.

Mafanikio hayo pia wamewezeshaNamana za wateja kuongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 1.18 mwaka 2021 kutoka shilingi trilioni 1.04 huku mikoponayo ikiongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 718.6 kutoka bilioni 617.81

Tanzania Commercial Bank TCB imekuwa ikifanya kazi na wafanyabiashara kuanzia  mfanyabiashara mdogo, wakati na mkubwanakuhakikisha kila mwananchi anapata huduma kutoka benki ya TCB kila kona  ya Tanzania na mipaka yake.

Previous articleSERIKALI KUTATUA MGOGORO KIWANDA CHA KATANI JIJINI DAR
Next articleSIMAMIENI SHERIA ZA UHIFADHI – WAZIRI BALOZI PINDI CHANA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here