PICHA ZOTE NA: TCRA
Na: Mwandishi Wetu.
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa vyombo vya habari mtandaoni vinatakiwa kujenga uimara wake katika kutangaza maudhui ya kujenga jamiii kwa kuandaa vipindi vilivyo bora.
Akizungumza katika Semina ya siku mbili ya Mafunzo ya Vyombo vya Habari vya Mtandaoni Mwenyikekiti wa Kamati hiyo Habbi Gunze amesema kuwa maudhui lazima yazingatie weledi na sheria kwanii vyombo hivyo ili kuleta tija kwa jamii.
Amesema kuwa Teknolojia inakwenda kwa kasi hivyo vyombo vya habari mtandao vifanye kazi kuelimisha jamii na kuacha kuwa sehemu ya kupotosha na kwamba sheria itatumika kudhibiti hali hiyo.
“Tutakwenda pamoja katika kutoa elimu katika kuhakikisha mnasimama na matokeo yake jamii itaelimika huku maendeleo yakionekana kutokana na kupata habari zinajenga zaidi” amesema Gunze
Mjumbe wa Kamati ya Maudhui wa TCRA Dereck Mrusuri amesema kuwa vyombo vya habari mtandao vinatakiwa kubadilisha mtazamo wa kufanya kazi hiyo kwa kuwa na vipindi vinavyojenga na hatimae kuwa na uwezo wa kifedha na kujiendesha.
Amesema kuwa kuna watu wamefanikiwa vizuri katika kutengeneza vipindi vinavyojenga na jamii ikafuata na kupata mabadiliko ya kiuchumi kutokana na chombo cha habari kujikita katika kutatua changamoto ndani ya jamii.
Aidha amesema kuwa katika kufanya kazi kwa ustadi kwa vyombo vya habari kupitia waandishi kuzingatia masuala ya uvaaji kwani wakati mwingine mtu anaweza kudhalaulika kutokana na mavazi.
Mkuu wa Kitengo cha Leseni za Mawasiliank wa TCRA Mhandisi Andrew Kisaka amesema kuna TV za mitandaoni kazi yake kuchukua vipindi vya nje ya nchi wakati leseni yake amechukua TCRA.
Amesema kuwa vipindi vingi watu wanatumia lugha ya kiingereza wanakwenda katika kutoa elimu kutumia lugha ya kiswahili kwani kiswahili kina maneno yakwenda kukidhi matamanio ya watazamaji.
Semina hiyo ya siku mbili imefanya Mei 18 na 19,2022 katika ukumbi wa mikutano wa TCRA Jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na washiriki zaidi ya 100 wakiwemo washiriki kwa njia ya mtandao kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.