Home BUSINESS NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AKAGUA ENEO LA MRADI WA LNG

NAIBU KATIBU MKUU NISHATI AKAGUA ENEO LA MRADI WA LNG

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (wa kwanza kushoto), akitoa maelekezo kwa Watedaji wa Wizara hiyo na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), alipowasili katika eneo litakalojengwa mradi wa kusindika gesi asilia (LNG), Likong’o Mkoani Lindi Aprili, 02, 2022.


Kamishna msaidizi wa Mafuta na Gesi wa Nishati nchini, Mhandisi Mohammed Fakih akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (wa pili kulia), wakati wa ziara ya kukagua eneo hilo lililopo Likong’o Mkoani Lindi, Aprili, 02, 2022.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali (kulia) akionyeshwa mchoro wa ramani ya eneo litakalojengwa mradi wa kusindika gesi asilia (LNG), na Mjiolojia mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Simon Zabron, wakati wa ziara ya kukagua eneo hilo lililopo Likong’o Mkoani Lindi, Aprili, 02, 2022.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, akikagua sehemu ya mabomba ya gesi asilia katika kituo cha makutano ya kuunganisha gesi hiyo inayotoka Mtwara na Songosongo Mkoani Lindi, mara baada ya kutembelea kituo hicho kilichopo katika Kijiji cha  Somangafungu Mkoani Lindi  Aprili, 02, 2022.

Na: Zuena Msuya, Lindi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali ametembelea na kukagua eneo la Likong’o litakalojengwa Mradi wa kusindika Gesi Asilia (LNG) na eneo la makutano ya kuunganisha gesi inayotoka mkoani Mtwara na Songosongo mkoani Lindi.

Akiwa katika ziara hiyo amewaasa watendaji wa maeneo hayo kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kuzingatia manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla

Katika ziara hiyo ya kikazi, Mahimbali aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, Kamishna Msaidizi wa Mafuta na Gesi kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Mohamed Fakih, na Meneja wa Kiwanda cha kuchata gesi asilia cha Madimba, Mhandisi Sultan Pwaga, pamoja na maafisa wengine kutoka wizarani na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Ziara hiyo imefanyika Aprili 2, 2022 mkoani Lindi.

Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara yake aliyoianza Machi 31, 2022 kwa kukagua mradi wa gesi wa Songosongo mkoani Lindi, kisha Aprili 1, 2022 alikagua kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba, visima vya gesi katika eneo la Mnazi Bay pamoja mradi wa usambazaji wa miundombinu ya gesi asilia kwa matumizi 

Previous articleMAKAMU WA DKT. MPANGO AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2022
Next articleSERIKALI KUWAPA BIMA WASHINDI WA TUZO ZA MUZIKI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here