Home LOCAL MAKAMU WA DKT. MPANGO AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2022

MAKAMU WA DKT. MPANGO AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa kwa mwaka 2022, Tahili Nyandabara mara baada ya kuuwasha na kuzindua mbio hizo,hafla iliofanyika katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe leo tarehe 2 Aprili 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 2 April 2022 akiwasili katika uwanja wa Sabasaba uliopo Mkoani Njombe  kwaajili ya kuzindua mbio za Mwenge kwa mwaka 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia hadhara iliojitokeza katika uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022, hafla iliofanyika katika uwanja wa Sabasaba uliopo Mkoani Njombe  leo tarehe 2 April 2022.Vijana wa halaiki wakifanya maonyesho wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Sabasaba Mkoani Njombe tarehe 1 April, 2022 Mbio hizo zimezinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Mpango   tarehe 02 Aprili, 2022.

Vijana sita waliondaliwa kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, wataukimbiza Mwenge wa Uhuru katika mikoa 31 na halmashauri 195 nchini kwa siku 195, wakiwa katika hali ya ukakamavu wakati wa  kuzindua mbio za Mwenge huo katika uwanja wa Sabasaba uliopo Mkoani Njombe  leo tarehe 2 April 2022.

 Baadhi ya wananchi wakifuatilia shughuli za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2022 katika uwanja wa Sabasaba uliopo Mkoani Njombe  leo tarehe 2 April 2022.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

KAZI, VIJANA , AJIRA NA WENYE ULEMAVU

 

Na: Mwandishi Maalum.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor  Mpango amezindua Mbio  za Mwenge, katika  viwanja vya Saba saba, mkoani Njombe.

 

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, tarehe 2 Aprili 2022, Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mpango ameeleza kuwa Mbio hizo zitakagua shughuli za Maendeleo na kumulika miradi.

 

Aidha, ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kukamilisha uchunguzi wa miradi 52 ya maendeleo  ambayo haikuzinduliwa wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa  mwaka 2021.

 

 Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema kuwa TAKUKURU wanatakiwa kuhakikisha wanakamilisha miradi iliyokuwa imekataliwa wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 baada ya kukutwa na dosari.

 

“TAKUKURU katekelezeni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan la kukamilisha uchunguzi wa miradi 52 iliyokuwa na dosari na haikuzinduliwa katika Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 na endapo kuna ushahidi wa kutosha basi waliohusika  muwafikishe Mahakamani” Amesema Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mpango.

 

Aidha, amewataka wanaokimbiza Mbio za Mwenge kwa mwaka huu kuhakikisha wanakagua na kuzindua miradi ya maendeleo iliyo katika viwango vinavyotakiwa.

 

“Hakikisheni miradi mtakayozindua inalingana na thamani ya fedha iliyotumika na endapo kutakuwa na changamoto toeni taarifa katika mamlaka inayohusika ili miradi hiyo ifanyiwe uchunguzi.” Alisisitiza Makamu wa Rais.

 

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mpango ameiagiza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kuendelea na mipango na mikakati yake ya kudhibiti na kuzuia dawa hizo nchini.

 

“Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya endeleeni na operesheni za ukamataji wa dawa za kulevya kwenye maeneo ya mipakani  na nasisistiza muwe mnakamilisha uchunguzi na kuchukua hatua za nidhamu kwa wote wanaohusika” Amesisitiza Makamu wa Rais.

 

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa baada ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 vijana sita waliondaliwa kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, wataukimbiza Mwenge wa Uhuru katika mikoa 31 na halmashauri 195 nchini kwa siku 195.

 

Aidha, Prof. Ndalichako alisema kuwa kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitaendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii ya Watanzania kuhusu umuhimu na uzingatiaji wa lishe bora, mapambano dhidi ya rushwa, ugonjwa UKIMWI pamoja na mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na Malaria.

 

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 zitafikia kilele chake Oktoba 14, 2022 mkoani Kagera zenye kauli mbiu Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo: Shiriki kuhesabiwa, tuyafikie Maendeleo ya Taifa ikiwa ni ujumbe uliozingatia hoja na vipaumbele vya Serikali ikiwemo umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 itakayofanyika Agosti 14, 2022.

 

Mwisho


Previous articleMAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AIAGIZA TAKUKURU KUKAMILISHA UCHUNGUZI WA MIRADI 52
Next articleNAIBU KATIBU MKUU NISHATI AKAGUA ENEO LA MRADI WA LNG
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here