Home LOCAL KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI KUTANGULIZA UZALENDO KATIKA...

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI KUTANGULIZA UZALENDO KATIKA MAJUKUMU YAO

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahil Geraruma akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nanungu(hawapo pichani)kabla ya kufungua vyumba vinne vya madarasa katika shule hiyo vilivyojengwa chini ya mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Covid-19, ambapo amewataka wanafunzi na walimu wa shule hiyo kutunza madarasa hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu,kushoto Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa.


Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa akikagua ubora wa madirisha katika mradi wa ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa shule ya sekondari Nanungu wilayani Namtumbo


Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nanungu wilayani Namtumbo wakiimba wimbo maalum wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika katika shule hiyo kwa ajili ya kufungua vyumba vinne vya madarasa vilivyojengwa chini ya mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Covid-19.


Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahil Geraruma akizindua mpango wa anuani za makazi ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,kushoto Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Vita Kawawa.

Picha na Muhidin Amri

Na: Muhidin Amri,Namtumbo

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Sahil Geraruma,amekeme tabia ya baadhi ya wataalam na watendaji wa Serikali kutanguliza  maslahi binafsi pindi wanapopewa dhamana ya kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Badala yake,amewataka kuwa wazalendo,waaminifu na kutambua kuwa nafasi walizonazo ni kwa ajili ya kuitumikia  jamii  na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha miradi kushindwa kuleta tija iliyokusudiwa.

Geraruma ametoa kauli hiyo jana,mara baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika shule ya Sekondari Nanungu Halmashauri ya wilaya Namtumbo vilivyojengwa chini ya mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Covid -19.

Alisema,kuna tabia imejengeka kwa  baadhi ya watendaji wa umma  kushindwa kusimamia na kutekeleza vyema miradi  kutokana na kasumba ya kutanguliza kwanza maslahi binafsi.

Alisema,hali hiyo imesababisha miradi mingi kujengwa chini ya kiwango na kushindwa kulingana na fedha zilizotolewa  na Serikali hivyo  kusababisha baadhi ya miradi kutodumu kwa muda mrefu.

Amewaagiza watendaji  waliosimamia ujenzi wa madarasa hayo kuhakikisha wanafanya marekebisho ya kasoro ndogo ndogo zilizojipo ikiwamo sehemu ya fishabodi ili wanafunzi waendelee  kuyatumia mara shule  zitakapofunguliwa.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa hayo  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Namtumbo,Mkuu wa shule hiyo Judith Ndomba alisema serikali kuu ilitenga kiasi cha Sh.milioni 80,lakini hadi kukamilika kwake wametumia Sh.79,660,500.

Ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake za kuboresha elimu hapa nchini kwa kujenga mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.

Previous articleWAKAZI WA NYASA WAJITOKEZA KWA WINGI KWENYE KAMPENI YA UCHUNGUZI WA KIFUA KIKUU
Next articleWAKANDARASI,MIRADI YA MAJI WAISHUKURU SERIKALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here