Home BUSINESS MKE WA MAKAMU WA PILI WA RAIS SHARIFA OMAR KHALFAN AYAFUNGA MAFUNZO...

MKE WA MAKAMU WA PILI WA RAIS SHARIFA OMAR KHALFAN AYAFUNGA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI ZANZIBAR

NA: MWANDISHI WETU.

MKE wa makamu wa Pili wa Rais Zanzibari Sharifa Omar Khalfan, leo amefunga mafunzo ya ujasiriamali ya Mwanamke Fanikisha yaliyokuwa yakiendesha kwa muda wa wiki moja na watoa mada tofauti katika ukumbi wa Abla apatiment.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi, kwa ajili ya kuelimisha wanawake ili kuweza kuendesha biashara zao ikiwa ni moja kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Katika semina hiyo wajasiria mali wamefundishwa jinsi ya kulinda afya zao, Usafi wa mwili pamoja na mazingira kwa ujumla, kukuza mitaji yao, jinsi ya kuanzisha biashara.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mke wa Makamu wa Pili wa Raisi Sharifa Omar Khalfan, ameahidi kushirikiana na mkuu wa wilaya kuwafiki wajasiriamali waliopatiwa mafunzo hayo.

“Tunatakiwa kushikana mikono ili kufikia malengo katika biashara zetu nitaungana na Mkuu wa Wilaya Suzan Peter Kunambi, kuwafikia wote mlipata mafunzo haya ili kuboresha biashara zenu kulingana na mafunzo mliopatiwa,” anasema Sharifa Omar Khalifan.

Kwa upande wa muandaajia wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi, amewataka wajasiriamali hao kuunda vikundi kwa ajili ya kuwapatia mikopo ya kuendeleza biashara zao.

“Niwapongeze wote walioshiriki katika mafunzo haya hatua inayofwata muende mkaanzishe vikundi ambavyo tutakuja kuwa wezesha kwa ajili ya kuboresha biashara zenu.”

Mafunzo hayo yali hitimishwa na watoa mada mbunifu Martn Kadinda, Shande Yussuph na Mkuu wa Wilaya Suzan Peter Kunambi.

Previous articleMASANJA AWAONGOZA WANAWAKE 500 KUTEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO.
Next articleMARTIN KADINDA AWAPA NENO WANAWAKE NA VIJANA WAJASIRIAMALI KISIWANI ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here