Home BUSINESS MASANJA AWAONGOZA WANAWAKE 500 KUTEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO.

MASANJA AWAONGOZA WANAWAKE 500 KUTEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO.



Naibu waziri wa wizara ya maliasili na utalii Marry Masanja akiwa katika gari la kitalii tayari kwa safari ya kuelekea hifadhi ya Ngorongoro.


Mkuu wa mkoa wa Arusha akiongea na wanawake katika eneo la ofisi yake wakati wa kuanza safari kuelekea hifadhi ya Ngorongoro kwa wanawake zaidi ya 500.


Mkuu wa mkoa wa Arusha akiongea na wanawake katika eneo la ofisi yake wakati wa kuanza safari kuelekea hifadhi ya Ngorongoro kwa wanawake zaidi ya 500.


Naibu waziri wa wizara ya maliasili na utalii Marry Masanja akiwa amembeba Sharon Ringo balozi wa utalii jumuiya ya Afrika Mashariki.

Baadhi ya wanawake walipoenda kutembelea hifadhi ya Ngorongoro kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

NAIBU  waziri  wa Maliasili na Utalii Marry Masanja amewaongoza zaidi ya wanawake 500 kwenda kutembelea mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambapo pia  ni sehemu ya  kuhamasisha utalii wa ndani.

Akiongea wakati wakianza safari hiyo  katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Masanja amesema kwamba tukio hilo ni kuunga mkono juhudi alizoanza Rais Samia Suluhu Hassan ambapo alisema wamechagua wiki hii ya wanawake Duniani kuionyesha Afrika na Dunia kwa ujumla na kuwakumbusha watanzania kwamba wao ni wajenzi wa taifa lao.

“Na kujenga kwetu ni kwa vitendo  ambapo tunapoenda kuona vivutio sio kwa kutazama tuu lakini pia kwa kujifunza kwani Kuna mambo mengi ya kujifunza vikiwemo viumbe hai pamoja na fuvu la mwanadamu wa kwanza ambalo huwezi kulikuta sehemu yoyote Duniani,”Alisema Masanja.

Alifafanua kuwa wanaamini Ngorongoro ni bustani ya Eden hivyo wameona katika maadhimisho ya siku ya wanawake hawawezi kukosa kwenda ambapo pia Alieleza kuwa suala la kukuza utalii wa ndani linaanza na mtu mmoja mmoja lakini pia  ni sehemu ya kutekeleza na kuunga mkono juhudi za Mh.Rais wetu ambaye amekuwa mshiriki namba moja wa kutangaza utalii wetu.

“Nifuraha kubwa kuona kundi hili la kinamama waliojitokeza kuunga mkono suala zima la kukuza utalii wa ndani na wanawake wanaweza kuukuza utalii wa ndani na waneonyesha kwa vitendo kwa kulipa fedha zao kutembelea hifadhi ya Ngorongoro”

Awali akizungumza katika tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela alisema kuwa  Jana kazi imeanza na leo wanaenda kutembelea hifadhi ya Ngorongoro ambapo wakiwa katika matembezi haya watambue kuwa muongozaji wao namba moja ni Rais Samia Hassan Suluhu.

“Tanzania imefunguka,Arusha imefunguka,Samia Suluhu kazi iendelee, kazi hii Rais wetu yeye ndiye aliyeanza juhudi hizi  na nyie ni wasaidizi wake katika hili lakini pia nichukue fursa hii kuwapongeza wanawake wote,Alisema Mongela.

Kwa upande wake balozi wa utalii wa jumuiya ya Afrika Mashariki Sharon Ringo alisema kuwa anayofuraha kubwa sana ya kuwa sehemu ya kuutangaza utalii  wa ndani kwenda kujionea kivutio na Eden.

Alisema kwamba sio wanaume pekee yao wanaweza kufanyakazi hata wanawake wanaweza nazikawa msaada mkubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Previous articleSIMBA SC YAIADHIBU BIASHARA 3-0 KWA MKAPA
Next articleMKE WA MAKAMU WA PILI WA RAIS SHARIFA OMAR KHALFAN AYAFUNGA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here