Home ENTERTAINMENTS MARTIN KADINDA AWAPA NENO WANAWAKE NA VIJANA WAJASIRIAMALI KISIWANI ZANZIBAR

MARTIN KADINDA AWAPA NENO WANAWAKE NA VIJANA WAJASIRIAMALI KISIWANI ZANZIBAR

Martini Kadinda awang’ata sikio wanawamke wajasiriamali kisiwani Zanzibari

NA: MWANDISHI WETU

MBUNIFU nguli wa mavazi nchin Martin Kadinda amewataka wanawake wajasiria mali na vijana wa wilaya ya Magharibi ‘A’, kisiwani Zanzibari, kutumia utofauti alio nao binafsi kuboresha biashara yake.

Maritni ni miongoni mwa wabunifu wajasiriamali walio fanikiwa na kutambulisha taifa katika sekta ya mavazi na kujitwalia tuzo sita za kimataifa.

Akizungumza na wanawake wajasiriamali, katika kilele cha mafunzo ya Mwanamke Fanikisha, amesema kila mtu ameubwa na utofauti wake ni vizuri kutumia utofauti huo kutofautisha biashara yake.

“Binadamu wote ni sawa ila kila mmoja ameubwa na utofauti wake tunaweza kufanya biashara moja ila ukaitofautisha na nyengine kulingana na utofauti ulio nao binafsi ikavutia wateja wengi kwa sababu kila mtu ana kitu kinachomvutia na kukipenda,” anasema Martin Kadinda.

Aliongeza kwa kutoa mfano wote mnaweza kukaanga mihogo mmoja akaweka chachandu ya mbilimbi mwengine akaweka ya embe hapo tayari  mmesha tofautisha biashara zenu kila mmoja atakuwa na wateja wake.

Aidha alisema Zanzibar ni kisiwa ambacho kina frusa nyingi za biashara hasa kwa wanawake kwa sababu kuna wageni wa kitalii wengi tofauti na Tanzania Bara.

“Tunapaswa kutumia frusa ya wageni kutoka nchi tofauti kujikwamua kwa kubuni biashara ambazo zitawavuta zaidi watalii niombe serekali kuandaa tamasha kama hili ambalo litawaleta wakufunzi wengi kuja kutoa elimu kwa wanawake wa Zanzibari.

Previous articleMKE WA MAKAMU WA PILI WA RAIS SHARIFA OMAR KHALFAN AYAFUNGA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI ZANZIBAR
Next articleWAZIRI UMMY: SEKTA YA AFYA ITAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA UTENGAMAO NA KUWAWEZESHA WALEMAVU KUMUDU MAISHA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here