Home LOCAL MIILI YA WAANDISHI WA HABARI YAAGWA JIJINI MWANZA

MIILI YA WAANDISHI WA HABARI YAAGWA JIJINI MWANZA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nauye akizungumza mbele ya Wombolezaji waliofika kuaga miili ya wanahabari watano katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza.

MWANZA.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nauye ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuchambua matukio yote ya ajali za barabarani kwenye misafara ya viongozi nchini ambayo yanachukua maisha ya wana tasnia hiyo.

Amesema hayo wakati akitoa pole kwenye hafla ya kuaga miili ya wanahabari waliopoteza maisha kwenye ajali iliyotokea jana Jijini Mwanza.

“Nilipokuwa nakuja huku wakubwa wangu wamenielekeza kuwa nifuatilie hili la ajali kwenye misafara ya viongozi,kwanini waathirika wamekuwa ni waandishi wa habari,lazima tujue chanzo ni nini?”,amesema.

Waziri Nape amesema baada ya kukabidhiwa taarifa ya uchunguzi mambo mengine yatafuata ikiwemo kubadilisha utaratibu mzima.

Amesema utaandaliwa utaratibu maalumu au itifaki rasmi ya namna bora ya ushiriki wa wanahabari kwenye ziara hizo.

Kauli hiyo ya Nape imejibu kilio cha Wanahabari wengi nchini kuwa mara nyingi hawapewi kipaumbele kwenye ziara hizo, ambapo mara nyingi wanapewa magari yasiyo na viwango, ambayo hayawezi kuendana na mwendo wa misafara yenyewe na kujikuta yakiachwa nyuma na pale wanapojitahidi kukimbia ili kuwahi matukuio wanaishia kupata ajali na kupoteza maisha.
Credit -Malunde 1 Blog.
Previous articleNAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. MOLLEL ASHIRIKI SHUGHULI YA KUAGA MIILI YA WAANDISHI JIJINI MWANZA
Next articleRAIS DKT. AONGOZA SHEREHE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here