Home LOCAL WANAFUNZI 3,404 KUANZA KIDATO CHA KWANZA KWA AWAMU MOJA MKALAMA

WANAFUNZI 3,404 KUANZA KIDATO CHA KWANZA KWA AWAMU MOJA MKALAMA


Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Wanafunzi 3,404 waliofauli darasa la saba katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wanategemea kuanza kidato cha kwanza kwa awamu moja kutokana na ujenzi wa madarasa 47 yanayojenhwa katika Halmashauri hiyo.

Akiwa ziarani Wilayani humo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amekagua ujenzi wa vyumba 7 vya madarasa katika shule ya Sekondari Gumangwa kwa niaba ya vyumba vyote 47 vilivyojengwa katika Halmashauari hiyo.

Kutoka katika mradi wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambamo dhidi ya UVIKO-19 Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imepoeka shilingi Milioni 940 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 47 katika shule za Sekondari Wilayani humo.

Akiwa shuleni hapo Waziri Ummy ameridhishwa na ujenzi wa madarasa hayo na amepongeza Uongozi wa Manispaa ya Singida kwa usimamizi makini wa ujenzi wa madarasa hayo.

Naye Makamu Mkuu wa shule ya Sekondari ya Gumangwa Mwl. Lucas Egugu amesema wanafunzi waliomaliza kidato cha nne katika shule hiyo ni 77 na waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza ni 245 lakini kwa ujenzi wa madarasa hayo 7 yatapawezesha wanafunzi wote kuanza kidato cha kwanza kwa awamu moja.

Pia amemshkuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa fedha walizopata kwa kuwa zimeongeza fursa za Elimu kwa watoto wote wa Kitanzania kupata elimu yao kwa wakati.

Previous articleNIC WAZINDUA PROMOSHENI YA “JIKAVE NA NIC”
Next articleBILIONI 48.5 KUKAMILISHA UJENZI NA KUNUNUA SAMANI ZA VYUO 25 VYA UFUNDI STADI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here