Home SPORTS PABLO: TUNAHITAJI POINT 3 DHIDI YA RUVU

PABLO: TUNAHITAJI POINT 3 DHIDI YA RUVU

 

Na: Mwandishi wetu

KOCHA mkuu wa Mabingwa watetezi Simba Pablo Franco amesema kuwa anahitaji kupata alama tatu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu shooting utakaopigwa ijumaa ili kuonheza hali ya kujiamini katika kikosi.

Kauli hiyo ameitoa leo uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere kabla ya kuelekea mwanza tayari kwa mchezo huo utakaocheza  katika dimba la CCM Kirumba Mwanza.

Pablo amesema ingawa hajapata muda mrefu wa kufanya mazoezi pamoja na wachezaji lakini anaamini atapambana kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu.

Ameongeza kuwa kirejea kwa nyota ambao walikuwa katika timu ya taifa kumeongeza nguvu kikosini na kuelekea katika mtanange huo.

“Kikubwa tunahitaji kupata alama tatu katika mchezo dhidi ya Ruvu shooting, ninajua mchezo utakuwa mgumu na upinzani utakuwa mkubwa lakini ushindi ndio kitu tunachokihitaji ili kirudisha hali ya kujiamini “ amesema.

Hata hivyo mchezo huo utakuwa wa kwanza wa kocha Pablo tangu alipotua kuchukua mikoba ua Didier Gomes.

Previous articleSENSA YA MAKAZI NA WATU KUFANYIKA KIDIGITALI
Next articleYANGA YAAHIDI KUICHAPA NAMUNGO KWAO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here